Menu

05. Ukweli

Habari si sayansi halisi. Hakuna ukweli unaothibitishwa kisayansi. Hii inamaanisha kwamba hakuwezi kuwa na kutoegemea upande mmoja wakati wa kuandaa habari. Habari zote ni matokeo ya mitizamo ya kibinadamu, bila kujali muundo wa kiuandishi uliotumika kuzisambaza. Uhusikaji wa mwandishi wa habari unapaswa kuchukuliwa kama hakikisho la uadilifu.

HESHIMU UKWELI ULIOCHUNGUZWA… LAKINI KUWA MAKINI

Kuheshimu ukweli uliochunguzwa si suala la kuripoti tu kwa usahihi. Unapaswa pia kuelezewa kwa mtiririko, kuwekwa kwa muktadha, juhudi lazima ifanyike kuelezea kwa nini jambo hilo lilitokea, ikiwezekana, unapaswa kuelezewa kwa uthabiti. Hii inahitaji uchunguzi makini wa ukweli, badala ya uchunguzi wa juu juu.

Ukweli unaoelezewa hovyo hovyo, nje ya muktadha au wakati tukio bado liko motomoto unaweza kujumuisha uongo endapo utakuwa tu na kipande cha ukweli. Anapokuwa na shaka mwandishi mwadilifu anakiri kutoelewa kwakehatuna uhakika kabisa wa nini kilichotokea.

HESHIMU MAELEZO YA MASHUHUDA… BILA KUKUBALIANA NAYO

Kuheshimu maelezo ya mashuhuda si tu suala la kuyaripoti bila kuyapotosha. Lakini pia ni kumhabarisha msomaji mazingira ya upatikanaji au kuombwa kwake, mashuhuda ni kina nani na ni kwa namna gani maelezo yao yana uhalali. Ikiwa maelezo hayo ya mashuhuda yanaambatana na nadharia, mwandishi wa habari hapaswi kuwapa wasomaji wake mwonekano kwamba yeye mwenyewe binafsi anayaamini.

Ingawa wakati mwingine maelezo yanaweza kupunguza ubora wa habari, tahadhari inabidi kuchukuliwa katika uandishi ili kuepuka kutoeleweka: Kulingana na shuhuda huyu… Shuhuda huyu anadai kwamba… Bwana X aliona kila kitu: “Nilikuwepo” alisema… “Niliona…”.

HESHIMU MAONI… BILA KUYAKUMBATIA

Waandishi wa habari wanaandika maoni yote, hata yale wasiyoyapenda, lakini hawayaungi mkono. “Habari” kutoka vyanzo vya taasisi (taarifa kwa vyombo vya habari, maazimio, nk.) zinapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari sawa tu na zile zinazotoka katika vyanzo vingine.

Umma una haki ya kutegemea mwandishi wa habari kuelezea “kwa nini” na “jinsi gani” watu wanaotoa habari wanataka isambazwe, pamoja na madhumuni yao. Daima  kuwa makini. Tumia mipangilio sahihi (vichwa vya habari vinavyoonekana vizuri, aya ya kwanza ya habari yenye maelezo ya kutosha, nk.) ili kuepuka kutoa mwonekano kwamba gazeti linaunga mkono maoni rasmi ya chanzo cha habari.

Ikiwa msemaji wa Benki ya Wafanyakazi atachapisha tamko rasmi lenye kichwa cha habari kisemacho: “Mustakabali wa Benki ya Wafanyakazi ni mzuri kuliko wakati wowote ule”, linapaswa kuchapishwa chini ya kichwa cha habari kisichofungamana na maoni hayo. Kwa mfano, weka nukuu kati ya alama za kunukuu kuweka wazi kwamba kauli hiyo ilitolewa na benki peke yake na si gazeti lililoichapisha. Benki ya Wafanyakazi inahakikisha mustakabali wake “ni mzuri kuliko wakati wowote ule”.

KANUNI KUU: KAA MBALI

“Mbinu ya uandishi wa habari” ni kukaa mbali linapokuja suala la mitizamo, hisia za watu wengine na hisia zako mwenyewe. Kama mwandishi wa habari, unahitaji kujiweka katika nafasi ya msomaji na kujiuliza: Je, kile nachokindika na maoni nayotaka kuyaelezea yataeleweka na wale watakaoyasoma?

Ikiwa utakuwa hata na shaka kidogo tu, andika habari yako upya.