Menu

18. za thamani ya

Maudhui ya habari daima yanaweza kuboreshwa. Daima kuna jambo unaloweza kufanya ili kuifanya habari yako kuwa sahihi zaidi, fupi zaidi, kamili zaidi, na inayovutia zaidi. Waandishi wa habari makini daima hutafuta kuiongezea kazi yao thamani. Muda unaweza kubana, lakini bado kuna nafasi: maudhui yanaweza kuongezwa hadi dakika za mwisho mwisho kabisa.

MABORESHO YA MWISHO-MWISHO

* Unapotaja jina la ukoo la mtu, hakikisha pia unataja jina lake la kwanza, kuepuka kutotofautisha majina ya watu yanayofanana: “Mark Mahela…”.

* Unapotaja jina la mwanasiasa, hakikisha pia unataja kazi yake na chama chake cha siasa kwa vile ni mtu mashuhuri: “Said Salim, Mbunge wa wa Takachao kwa tiketi ya…”.

* Unapomtaja mtu kwa mara ya kwanza, angalau taja umri na kazi yake: “Vivian Momba, 40, afisa ugavi…”.

* Unapotaja kifupi cha jina kwa mara ya kwanza, elezea maana yake kwa kutilia maanani wasomaji ambao wanaweza wasielewe maana yake. “Umoja wa Afrika (AU)”

* Ukiandika habari kuhusu matukio ya kihistoria au mambo yaliyotokea zamani, tumia vielezi-chini (footnotes) kuwakumbusha wasomaji wazee na kuwaelemisha vijana: (1) “Mark Mahela, mfanyabiashara wa Kitanzania na mtaalamu wa masuala ya benki na mwanzilishi wa Benki ya Wafanyakazi, alizaliwa Dodoma mwaka 1963. 

MASWALI SAHIHI

 “Ni nini nachoweza kufanya vizuri zaidi?”  “Ni nini tunachoweza kufanya vizuri zaidi?”  “Ni nini unachoweza kufanya vizuri zaidi?”  Iwe ukijiuliza mwenyewe kwa jambo lako binafsi, uliza katika kikao cha idara au ikiwa ni swali lililoulizwa kwenye kikao cha kuandaa habari, maswali – nawezaje kuboresha uandishi wangu wa habari na nawezaje kuendeleza habari yangu – yana uwezekano wa majibu manne: mwegemeo kinyume, habari mbadala, habari kinzani, na habari ya kukazia

Mwegemeo kinyume. Uzuri wa kuandika habari ya mtizamo kinyume uko katika kutengeneza matokeo ya kulielezea jambo husika kinyume. Hii inahusisha kuandika nyongeza ya habari kuu kwa kuiandika kwa mwegemeo tofauti kabisa. Niliamua kuandika kupanda kwa haraka katika tasnia ya benki kwa Mark Mahela katika habari yangu kuu. Kwa habari ya mwegemeo kinyume, nitaandika pia matokeo ya uongozi wake kama mkuu wa Benki ya Wafanyakazi, ambao waajiriwa wanaamini umekuwa na madhara…

Habari mbadala. Uzuri wa habari mbadala uko katika kuelezea kilichopo nyuma ya pazia. Unaandika habari kuu sambamba na habari nyingine, ambayo inaweza kuwa tofauti kidogo ikilinganishwa na habari kuu. Niliamua kuandika habari yangu kuu kuhusu vikwazo vilivyoikumba Benki ya Wafanyakazi katika juhudi zake za kuhamishia makao makuu yake nje. Kwa habari mbadala, nitaandika wasifu na mahojiano na mmoja wa wawekezaji wa Benki hiyo, asiyejulikana kwenye jamii, mwenye jukumu la kutafuta maeneo na kusuluhisha migogoro yoyote ya kiutawala inayojitokeza kiutendaji…

Habari kinzani. Uzuri wa habari kinzani uko katika kuandika habari inayotoa taswira tofauti. Andika uchunguzi unaokinzana na uchunguzi wa awali, maelezo yanayokinzana na maelezo ya shuhuda, ripoti inayotofautiana na ripoti ya mtaalamu, mfano tofauti na mfano uliotolewa, nk. Mhariri wangu mkuu ameamua kupinga uchunguzi wangu mahiri kabisa kuhusu ujenzi wa jengo lenye usalama wa hali ya juu la Mark Mahela kwenye eneo la hifadhi kwa kuja na uchunguzi tofauti kutoka kwa mwandishi wetu maalum wa Kusini, ambao unaelezea uwekezaji kwenye mazingira uliofanywa na mmiliki huyo wa benki… sina pingamizi na hilo. Msomaji atajikuta ana maoni mawili yanayokinzana kuhusu utendaji wa Mark Mahela – ubaya wake kwa upande mmoja na uzuri wake kwa upande mwingine – na tutawaachia wasomaji ndiyo wawe waamuzi…

Habari ya kukaziaUzuri wa habari ya kukazia uko katika kuandika habari inayoimarisha habari kuu. Unaimarisha habari yako kuu kwa kuandika habari kadhaa za nyongeza. Nitaimarisha uchunguzi wangu kuhusu ujenzi wa jengo jipya lenye ulinzi wa hali ya juu la Mark Mahela kwenye eneo la hifadhi kwa kuongeza vipengele vitatu vyenye maelezo ya kina kwenye habari kuu: mahojiano mafupi (maswali 3 na majibu yake) na meya wa zamani wa Sinde, ambaye, baada ya kutochaguliwa katika uchanguzi uliopita, sasa yuko radhi zaidi kuelezea anachokijua; habari ndogo ndani ya habari ikielezea sheria zinazohusu maeneo ya hifadhi; na grafu inayoonesha maendeleo ya maliasili ya kisiwani hapo, ambayo sasa yako katika hatari kutokana na ujenzi huo mkubwa,…

KINGA YA MAJANGA NA HUZUNI INAYOSABABISHA NA HABARI.

Mara nyingi habari inahuzunisha kiasi kwamba waandishi wa habari makini daima hutafuta namna ya kuepuka kuifanya ionekane imejaa majanga na huzuni. “Kinga” bora kabisa ni kuongeza “tabasamu” kwenye zile kurasa zenye habari za huzuni sana. “Tabasamu” ni aina ya uandishi ulio katika mitindo mbalimbali, lakini ambao mara zote una maudhui ambayo kidogo, na kwa makusudi, yanaliwaza. Inaweza kuwa kibonzo, maoni, wasifu, mahojiano mafupi, maelezo ya shuhuda, nk. jambo muhimu ni kwamba inapaswa kuwa habari inayofurahisha kiasi cha kumfanya masomaji aliwazike, atabasamu, au acheke. Hii itakuwa ni wasifu wa muuza duka la rejareja ambaye anafurahia maisha yake licha ya uchunguzi unaoendelea kuhusu mgogoro husika. Itakuwa ni mahojiano na mtu anayeona kwamba ujenzi huo ni jambo zuri yatakayowekwa chini ya uchambuzi unaoonesha hilo ni janga. Au hata kibonzo cha dhihaka, nk.

THUBUTU KUACHANA NA MAZOEA.

Siku zote kuna wasomaji wapya wa kuwavutia. Gazeti linalowafahamu vizuri wasomaji wake linajua namna ya kutambua maeneo ya udhaifu wao. Hayo yakishabainishwa, mara nyingine inatosha tu kuleta mambo mapya ili kukonga nyoyo za wasomaji. Nimeongeza mauzo ya gazeti langu kwa siku moja kwa kuchapisha katikati ya kurasa za masuala ya siasa za ndani, safu ya kila wiki ya ushairi, shairi lililoandikwa na mwandishi mashuhuri katika kanda. Pia gazeti langu limepata wateja wapya tangia nilipochapisha barua za wasomaji zilizoandikwa kwa lugha yao.