Menu

02. Mikutano ya kuandika

Gazeti ni matokeo ya juhudi za pamoja. Kikao cha Chumba cha Habari ni kikao ambacho waandishi wa habari wanajadili kazi yao ya pamoja. Majadiliano hayo yana madhumuni matatu yanayofuatana: kupanga maudhui ya gazeti, kuratibu uzalishaji wa maudhui hayo na kutathmini maudhui yote ili kuyaboresha. Kwa hiyo, Kikao cha Chumba cha Habari kinaweza kutumika kwa magazeti yote na ratiba zote za uchapishaji.

KUNA AINA TATU ZA VIKAO VYA CHUMBA CHA HABARI:

  1. Kikao cha Chumba cha Habari kuandaa ushughulikiaji wa mambo yanayotokea kila siku.Wahariri wa gazeti la kila siku wanakuwa na kikao cha pamoja kila siku mchana ili kupanga maudhui ya gazeti la siku inayofuata. Wanaandaa “Orodha ya Muda ya Habari” kwa kila ukurasa: idadi ya habari, aina ya habari, urefu wa habari, mpangilio wa umuhimu wa habari, vielelezo.

 Mfano wa “Orodha ya Muda ya Habari” kwa ukurasa wenye safuwima 6: Habari 1 na X… (Safuwima 3); habari 1 kuhusu majadiliano + maoni 1 na Y… (Safuwima 2); mfululizo 1 wa Habari kwa ufupi (safuwima 1).

  1. Kikao cha Chumba cha Habari kupanga ushughulikiaji wa mambo yanayotokea kila siku.Wahiriri wa gazeti la kila siku wanakutana kila asubuhi ili kupanga maudhui ya gazeti linalochapishwa siku inayofuata. Wanagawana kazi kati yao ili kuandaa “Orodha ya Jumla ya Habari”, ambayo itakuwa “Orodha ya Habari Iliyokamilika”: orodha ya habari, majina ya waandishi, urefu uliowekwa kwa kila habari.

Mfano wa “Orodha ya Habari Iliyokamilika” kwa ukurasa wenye safuwima 6: Habari 1 na X… (Safuwima 2¼ za maneno + safuwima 3/4 picha); habari 1 kuhusu majadiliano (safuwima 1½) + Maoni 1 na Y… (Safuwima ½); Habari kwa ufupi 4: Mahakamani, Polisi, Uchumi, Masahihisho ya habari iliyopita (safuwima 1).

  1. Kikao cha Chumba cha Habari kutafakari ushughulikiaji wa mambo yanayotokea kila siku.

Wahariri wa gazeti la kila siku wanatenga muda wa kukutana mara kwa mara – kwa mfano, mara moja kwa robo au mara moja kila baada ya miezi sita – ili kushirikiana katika kutathmini, kujikosoa, kazi yao ya pamoja kwa kipindi cha miezi michache iliyopita na kutafakari kwa pamoja ili kupata namna nzuri zaidi ya kushughulikia habari siku za usoni na kuamua misimamo ambayo gazeti itachukua. Kisha Kikao cha Chumba cha Habari kinakuwa Kamati ya Uhariri, ambayo inaweza kuitishwa kwa mapendekezo ya pamoja ya Mkurugenzi wa Gazeti, Mkurugenzi Mhariri au Mhariri Mkuu kwa ajenda mahsusi.

Mfano wa ajenda:

  1. Mapitio ya namna tulivyoshughulikia “Vuguvugu la Maandamano dhidi ya Serikali katika Nchi za Kiarabu Majira ya Kuchipua”.
  2. Maandalizi ya uchaguzi wa madiwani.
  3. Je, gazeti linapaswa kufungamana na upande mmoja kwenye uchaguzi ujao wa Rais?

VIKAO VYA KUSIMAMA

Kuzalisha gazeti kila siku ni sawa na kukimbizana na muda kila siku. Ili kupata muda, waandishi wa habari wanabaki wakiwa wamesimama wakati wa Kikao cha Chumba cha Habari kuhitimisha jinsi ambavyo watashughulikia habari wanazoziandaa tokea siku iliyopita. Kwa nini wanabaki wakiwa wamesimama? Kwa sababu kuwa wima ni njia ya uhakika zaidi ya kufupisha vikao.

VIKAO VYA KUKETI

Tunaketi kwa vikao vyetu ikiwa tuna muda wa kuongea. Hivyo ndivyo ilivyo pale Kikao cha Chumba cha Habari kinapofanyika kwa mtizamo wa kuweka matarajio yake kuhusiana na kazi kuanzia siku moja hadi inayofuata au kuanzia wiki moja hadi nyingine. Hivyo ndivyo ilivyo pia pale Kikao cha Chumba cha Habari kinapogeuka Kamati ya Uhariri.

MFANO WA RATIBA KATIKA CHUMBA CHA HABARI KILICHOPANGWA KWA IDARA

09:30 Vikao vya idara. Ushiriki wa lazima kwa waandishi wote wa habari. Washiriki wanabaki wakiwa wamesimama. Kila mmoja anatoa mchango wake wa habari kulingana na shajara zao binafsi. Habari inayopendekezwa inapimwa, yaani kufanyiwa tathmini kuhusiana na vielelezo au vibambo, mistari, safuwima au kurasa. Kulingana na shajara ya pamoja, Mhariri wa Idara anatenda kama kiunganishi kati ya wafanyakazi. Yeye anaamua juu Orodha ya Habari za Kila Siku zilizopendekezwa na timu yake.

 Mfano wa Orodha ya Habari za Kila Siku kwenye Idara ya Siasa:

* Ukurasa wa 9:

– Muhtasari na A.R. wa mkakati wa uchaguzi wa Waziri Mkuu: Safuwima 2, mchoro na J.P.

Maoni ya mgawanyiko Bungeni kwa wabunge wa viti vingi (R.B.) Safuwima ½.

Ripoti kuhusu Bunge (L.Z.) Safuwima 1.

Mahojiano na Spika wa Bunge (A.G.) Safuwima 1½.

Habari kwa ufupi: Safuwima 1.

* Ukurasa wa 10:

Ripoti ya kampeni ya uchaguzi inayoendeshwa na chama cha mrengo wa kushoto kabisa (A.C.) Safuwima 2, picha 1 na R.D.

Picha ya mgombea wa Chama cha Ukombozi (A.B.) Safuwima 1½, picha na J.B.).

Uchambuzi wa kura za wanawake (J.G.) Safuwima 1½.

Habari kwa ufupi: Safuwima ½.

10:00 Kikao cha Utendaji cha Chumba cha Habari, chini ya uenyekiti wa Mkurugenzi wa Gazeti, Mkurugenzi Mhariri au Mhariri Mkuu. Wawakilishi wanapaswa kuwepo kutoka Idara zote. Washiriki wanabaki wakiwa wamesimama. Kila Idara inawasilisha Orodha ya Habari zake za Kila Siku kwa zamu. Majadiliano yanazingatia tu uteuzi wa habari za kupewa kipaumbele ukurasa wa mbele, ambao ndiyo kivutio cha gazeti zima, na marekebisho yanayopaswa kufanywa kwenye ukubwa wa habari hizo. Kikao hiki hakidumu zaidi ya dakika 20. Kupitishwa kwa Orodha ya Habari ya Jumla, ambayo inakuwa Orodha ya Habari Iliyokamilishwa kama itakavyowasilishwa kwa Mhariri Msanifu Mkuu.

10:30 Kila Idara inajumuisha maamuzi yaliyoorodheshwa kwenye Orodha ya Habari ya Jumla katika kazi zake za kila siku.

17:30 Kila Idara inaandaa Orodha ya Habari ya Awali kwa siku inayofuata. Kila mwandishi wa habari anawasilisha mipango yake kwa Mhariri wa Idara. Mhariri huyo anaandaa orodha ya mipango yote na anatoa maamuzi yake ya awali.

18:00 Kikao cha Muda cha Chumba cha Habari. Kikao cha kuketi. Wawakilishi wanapaswa kuhudhuria kutoka kila Idara. Kila Idara inaelezea Orodha ya Habari zake ya Awali kwa siku inayofuata. Kikao hiki kiko wazi kwa wahariri wote waliopo. Kikao cha mduara kuhusiana na Orodha ya Habari ya Jumla ambayo inaandaliwa kwa sasa. Muda wa kikao hicho hutofautiana kulingana na wingi wa kazi wa wale wanaohusika.

NIDHAMU BINAFSI

Mapendekezo mawili kwa uendeshaji mzuri wa Vikao vyote vya Chumba cha Habari:

  • Kamwe usisahau kwamba u mwerevu zaidi katika kikundi kuliko ukiwa peke yako.
  • Usichanganye madhumuni: vikao vya chumba cha habari hufanyika tu kwa ajili ya maudhui ya gazeti. (Mada nyingine za majadiliano: tofauti za maoni, migongano, matatizo ya uhusiano, masuala ya vyama vya wafanyakazi nk. kimsingi hudhughulikiwa na vyombo vingine).