Menu

03. lugha ya kiufundi ya uandishi wa habari wa magazeti

Pale waandishi wa habari wabobezi wanapowasiliana wao kwa wao, wanatumia lugha ya fani hiyo ambayo ilianza wakati wa uvumbuzi wa matbaa huko Ulaya, lakini ambayo iliendelezwa katika taaluma zote zinazohusiana na habari na nje kabisa ya uandishi wa habari. Lugha hii mahsusi inatumia makundi ya maneno yanayoendana na hatua mfuatano za mchakato wa kuandaa uchapaji wa habari.

MNAPOONGEA LUGHA MOJA, MNAWEZA KUBADILISHANA UJUZI.

LUGHA YA USANIFU

Habari (“paper”, “copy”): habari iliyoandikwa kwa ajili ya uchapishaji.

Mwegemeo wa habari: namna ambavyo mada inaanza kuandikwa.

“Lead”: sentensi ya kwanza au aya ya kwanza, inayolenga kumvutia msomaji.

“Body”: simulizi ya habari yenyewe, mpangilio wa kurasa za ndani, ukubwa wa vibambo.

Sentensi ya mwisho: hitimisho la habari, sentensi ya mwisho, aya ya mwisho.

LUGHA YA MTINDO WA UANDISHI

Maoni: habari fupi ambayo mwandishi anatoa maoni yake.

Habari fupi: habari fupi sana isiyo na kichwa cha habari.

“Bulletin”: maoni yasiyo na jina la mwandishi yanayoelezea msimamo wa gazeti.

Habari zinazogusa jamii: habari za matukio mbalimbali

“Column”: habari inayotoka baada ya muda maalum, iliyoandikwa kwa kwa namna ya uandishi wa mwandishi mwenyewe.

“Correspondence”: habari iliyoletwa na mwandishi maalum

“Wire story”: habari kutoka mashirika ya habari.

Udaku: habari fupi ya mambo ya kijamii.

Maoni ya Mhariri: maoni yaliyoandikwa na mkurugenzi au mhariri mkuu wa gazeti, mwandishi wa habari kutoka chumba cha habari au wakati mwingine mtu anayependa kuandikia magazeti.

Uchunguzi: ufichuzi, uchambuzi na uchanganuzi wa taarifa iliyopatikana kutoka vyanzo mbalimbali.

“Box”: aya fupi inayochomekwa kwenye maandishi kati ya mistari miwili ili kuvuta umakini wa msomaji.

Mahojiano: simulizi inayoelezea mahojiano, yaliyoandikwa kwa muundo wa maswali na majibu.

“Seasonal article”: habari ya mara kwa mara inayoongelea mada moja.

Wasifu wa marehemu: ripoti ya daktari ya uchunguzi wa kifo .

Ripoti: habari na ushuhuda wa kile kilichoonekana na kusikika huko mitaani .

Tangazo-habari (advertorial): tangazo linalotolewa kama habari.

Kigongo (scoop): habari ya kipekee ambayo ndiyo kwanza imetokea.

LUGHA YA UHARIRI

Kionjesho (kicker):mstari mfupi kwa kawaida juu ya kichwa cha habari unaoelezea habari kwa kifupi .

Vichwa vya Habari: vipengele vyote vinavyotengeneza kichwa cha habari .

Kichwa cha habari: maneno makuu ya habari .

Kichwa kidogo: usaidizi kwa kichwa cha habari.

Kibwagizo (inter): kichwa kidogo cha habari kinachowekwa ndani ya habari.

Jina la mwandishi: majina kamili ya mwandishi yanayowekwa juu au chini ya habari, kwa kirefu au kwa kifupi…

Maelezo ya picha: maneno yanayoelezea kielelezo.

Umiliki wa picha: jina la mpiga picha.

LUGHA YA UHAKIKI

Kosekano: neno moja au kadhaa yanayokosekana katika habari.

Neno lililokosewa: kosa la uandikaji sahihi wa neno.

Marudio: kosa la uandikaji linalosababisha neno, mstari, sentensi, nk kujirudia.

Kubadilisha maneno: kugeuza au kuchanganya herufi za neno.

Herufi: herufi ndogo inayotumika kuelezea ukubwa wa habari; idadi ya herufi kwenye habari ni idadi ya herufi ikiwa ni pamoja na nafasi za wazi.

LUGHA YA USANIFU

Safuwima kamili: habari inayoandikwa katika safuwima moja bila ya kukatwa na vichwa vidogo vya habari.

Kisanduku: maneno yanayozungukwa na kisanduku.

Kingo: mstari mnene au wa vitone unaotumika kutengeneza visanduku, au kutenganisha habari au maoni.

Kijachini: sehemu ya chini ya ukurasa.

Mlingoti: sehemu ya maoni ya mhariri.

Kichwa: sehemu ya juu ya ukurasa.

Kutoka: mwendelezo wa habari kutoka ukurasa wa mbele kwenda ukurasa wa ndani.

Kiwiliwili: sehemu ya kati ya ukurasa

LUGHA YA “DIRISHA”

Kihamasishi: maelezo kwenye ukurasa wa mbele kuhusu habari iliyoko ndani.

Bendera: sehemu ya juu ya ukurasa inayoonesha, kwenye ukurasa wa kwanza, jina la chapisho, na, kwenye kurasa za ndani, jina la sehemu, tarehe na ukurasa.

Habari Kuu: habari kuu kwenye ukurasa wa mbele ambayo inaendelea ndani.

Bango: kichwa ha habari kikubwa kabisa kinachotoka mwanzo hadi mwisho wa ukurasa.

Masikio: nafasi zilizo juu ya kila upande wa masthead.

Ufito wa chini: kichwa cha habari kikubwa sehemu ya chini ya ukurasa.

LUGHA YA UZALISHAJI

Kumaliza kazi:  idhinisho la mwisho la kurasa kabla ya uchapaji

Kumalizia: usanifu wa mwisho wa ukurasa kabla ya  “kumaliza kazi”. 

Kipimo: ukadiriaji wa urefu wa habari.

Bamba: mwonekano kamili wa chapisho, unaoonesha habari na matangazo yalivyokaa kati ya ukurasa na ukurasa.

Mfano kamili: kurasa zote zilizoandaliwa.

L.S. (“Lala Salama”): ukurasa wa mwisho kuandaliwa wa gazeti.

Uthibitisho: mfano wa habari kamili iliyochapwa.

Karatasi: kipimo kikubwa zaidi kinachotumika kupima ukubwa wa habari; kina mistari 25 yenye herufi 60, pamoja na nafasi, yaani herufi 1500.

Nambari: nambari ya ukurasa.

Mfano: mfano wa ukurasa au gazeti zima.

Akiba: idadi ya habari zilizobaki bila kutumika.

Menyu: orodha ya habari zilizopendekezwa au kutunzwa au orodha ya kurasa zinazopaswa kukamilishwa.

Mpangilio: uwekaji wa vichwa vya habari, habari yenyewe, vielelezo na kingo za kurasa kama ilivyo kwenye mfano.

Muundo: mpangilio wa habari na picha kwenye ukurasa.

Umiliki: kisanduku chenye maelezo ya kisheria kuhusu umiliki na uongozi wa gazeti.

Habari motomoto: kurasa kwa ajili ya habari mpya kabisa.

Kurasa baridi: kurasa zinazoandaliwa  mapema.

Yaliyomo: muhtasari wa maudhui ya gazeti.

LUGHA YA MAKATAZO

 “Usiandike mkeka”: epuka kuandika habari kana kwamba unasuka mkeka…

“Usibwabwaje”: usitumie mistari 100 kuelezea kitu ambacho kingesemwa kwa mistari 10.

Usibuni mambo: kwa mwandishi wa habari kubuni habari ndiyo jambo la chini kabisa kulifanya.