Menu

24. wajibu wa kijamii wa mwandishi wa habari

Uandishi wa habari umevurgwa kwa sababu ya kuwepo kwa mifumo mingine ya upashaji habari kutokana na teknolojia mpya.  Hio ndiyo ubaya wa intaneti: leo kuna vyanzo vingi vya ‘habari’ sawa na  idadi ya watu kwenye mitandano ya kijamii, na kuna kuna watu wengi wasio na weledi wanaosambaza habari kuliko wanataaluma ya habari. Waandishi wa habari wa kweli wanahitaji kuinua viwango vya taaluma yao.

WAANDISHI WA HABARI WANATETEA TU MAADILI YA WOTE

Waandishi wa habari ni wahudumu wa jamii lakini si wanasiasa kwa tafsiri ya kawaida ya neno hilo, ingawa jukumu lao la kijamii lina uzito wa kisiasa. Maadili ya msingi wa kazi yao ya kiweledi ni maadili ya ulimwengu mzima: amani, demokrasia, uhuru, mshikamano, usawa, elimu, haki za binadamu, haki za wanawake, haki za watoto, maenndeleo ya kijamii, nk. Kwa hiyo kazi yao inachangia kuleta mabadiliko ya kijamii na kisiasa.

Wakati wakitetea maadili hayo ya kiulimwengu, waandishi wa habari huwa hawatetei maslahi ya moja kwa moja, kisekta, binafsi au yanayowagawa watu. Vinginevyo, wataishia kuvuka mipaka, kuweka rehani uhuru wao na kuwafanya wasomaji kutokuwa na imani na kazi yao ambayo wanaihusisha na uhuru wao.

Kama waandishi wa habari wakijiunga na chama cha siasa, ambayo ni haki yao kama raia, lazima waepuke kutumia nafasi yao kukinufaisha chama chao na, hasa, kupigia debe misimamo inayochukuliwa na vyama vyao katika magazeti yao. Maazimio ya waandishi wa habari yanazuia kupotoka kwa kuwazuia waandishi wa habari ambao ni wanachama wa chama cha siasa au chama cha kitaaluma hususan kutoshiriki kuandika habari kuhusu chama hicho cha siasa au cha kitaaluma.

UANDISHI WA MAONI NAO UNAZINGATIA KANUNI HIZO HIZO 

Mara nyingi inatokea kwamba waandishi wa habari wanaotetea maadili ya kibinadamu hujikuta wakipingana wazi wazi na mamlaka zinazovunja au kuwanyima watu haki hizo. Wakati mwingine wanalipa upinzani huo kwa gharama ya maisha yao. Hata hivyo, hata katika kipindi cha msongo mkubwa sana, hawawezi kuvunja kanuni hizi za maadili ambazo huwataka kuheshimu misimamo yote, imani zote, na aina zote za kujieleza, zikiwemo zile zinazolenga kufinya haki zao. Waandishi wa habari watetezi wanaozingatia maadili ya kiulimwengu wanafanya ni jambo la heshima kuwapa wapinzani wao nao fursa ya kusikika na kuonesha uvumilivu kwa misimamo yao katika uchambuzi na maoni yao.

KUNA MAAZIMIO MBALIMBALI YA REJEA: 

  • Azimio la Kazi za Kiweledi za Waandishi wa Habari wa Kifaransa (1918).
  • Kanuni ya Maadili ya Chama cha Waandishi wa Habari wa Marekani (1926).
  • Kanuni ya Maadili ya Umoja wa Kitaifa wa Waandishi wa Habari Uingereza (1938).
  • Azimio la Kanuni za Maadili ya Waandishi wa Habari la Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa Habari, lijulikanalo kama “Bordeaux Declaration” (1954).
  • Azimio la Haki na Wajibu wa Waandishi wa Habari, lijulikanalo kama “Munich Declaration” (1971).
  • Kanuni ya Magazeti Ujerumani (Pressekodex, 1973).
  • Azimio la Vyombo vya Habari la UNESCO (1983).
  • Azimio la Maadili ya Uandishi wa Habari la Baraza la Ulaya (1993).

“Mke wa Kaisari lazima asiwe na tuhuma zozote…”. 

Kama ilivyokuwa kwa Pompeia, mke wa pili wa Julius Kaisari aliyemtelekeza kwa sababu ya tuhuma za uzinzi, waandishi wa habari lazima nao wasiwe an tuhuma zozote. Wajibu wao kwa jamii unamaanisha kwamba uadilifu wao wa kiweledi kamwe haupaswi kutiliwa shaka. Jambo hilo si tu linahusisha kuheshimu faragha, kuheshimu utu wa mtu, kupinga mbinu za kilaghai, kukataa kutetea maslahi fulani kinyume na maslahi ya umma, bali pia makatazo ya aina yoyote ile ya kula njama au kukubali uonevu.

***

Mambo yote haya yanaweka viwango vya juu sana vya ubobezi katika uandishi wa habari, lakini hicho ndicho hasa kinachofanya hadhi ya waandishi wa habari kuwa kubwa, angalau kulingana na Seneca: “Magnam fortunam magnus animus decet”, “Akili kubwa huzaa utajiri mkubwa…