Menu

13. hadithi

Kuripoti huchukuliwa kama moja ya fani zinazoheshimika sana. Ni jambo zuri sana kwa uandishi wa habari. Ripoti nzuri huwezesha kupatikana kwa mjumuisho wa aina zote nyingine za uandishi wa habari. Zaidi, huhitaji mwandishi wa habari kuandika kwa muundo na maudhui yanayoendana na habari iliyoandikwa vizuri sana. Ni sanaa ngumu. Ambayo haivumilii watu wenye uwezo duni. Lakini inahitaji kuwa na umahiri wa mbinu zote za uandishi.

SIFA 8 ZA UANDISHI MZURI:

  1. Wazo zuri.

Ili kuwa na mvuto, kwanza unahitaji kuwa na wazo lako la kusimulia. Jambo la kwanza ni kutafuta HILO wazo zuri, ambalo magazeti mengine hayatakuwa nalo. Katika ulimwengu wa habari, mara nyingi utalipata wazo hilo kwa kwenda kinyume na wengine. Kwa hiyo, baada ya kutekwa, Mark Mahela aliamua kuhamisha makao makuu ya Benki ya Wafanyakazi kwenye jengo kubwa lenye ulinzi mkali analolijenga kwenye kisiwa kidogo chenye utulivu cha Sinde? Kila mmoja sasa akili yake imegeukia kwenye ukubwa wa mradi huo, maendeleo yake, na mabadiliko makubwa kwenye kisiwa hicho? Waandishi wa habari maalum kutoka magazeti mahalia na kitaifa wote wanaminika kwenda Sinde…? Lakini mimi? Nitaiangalia kwa mtizamo tofauti. Nitakwenda kwenye hicho kisiwa kujionea ni kwa namna gani wenyeji wanavyoishi katikati ya ujezi huo mkubwa. Napendekeza mpango wangu kwa mhariri wangu mkuu, ambaye tayari anaelekea kufurahishwa nao sana…

  1. Ukusanyaji mzuri wa taarifa.

Ili kwamba uweze kuelewa ni nini hasa utakachokiona utakapokwenda kwenye eneo hilo geni, lazima angalau uwe na taswira ya kile unachotegemea kukutana nacho…Na bado ni kama vile sifahamu chochote kuhusu kisiwa cha Sinde. Kwa hiyo, naamua kufanya utafiti kabla sijaenda kukutana na wakazi wa kisiwa hicho. Nisipofanya hivyo, najiweka katika hatari ya kukosa mambo mengi mazuri wakati nikiwa huko.

  1. Taswira na matokeo ya maisha ya kila siku.

Kuripoti ni kuhusu kuandika maisha ya kila siku. Najitahidi kuwafanya watu waongee nami, nafanya jitihada ya kuwatambua wale ambao ni rahisi kuongea, wale wenye habari za kuvutia zaidi, na wale walio katika nafasi za mamlaka. Nanukuu mambo mengi ya kile ninachokiona na kukisikia, narekodi mazungumzo yangu (kwa ridhaa ya wale ninaowahoji); kabla ya kila mahojiano, naandika maelezo ya kina ya kila mmoja wa wahojiwa wangu: jina la kwanza na la mwisho, umri, kazi, rangi ya macho, rangi ya nywele, mwelekeo wa tabia, nk. Nanukuu pia maelezo yote ya kina yatakayonisaidia kuwaonesha wakiwa katika mahojiano.

  1. Kelele, rangi, harufu

Kuripoti ni kuelezea hali watu wanayoiishi. Milangu yangu yote ya fahamu iko makini sana. Narekodi kelele, rangi na harufu ili niweze kuzielezea katika habari yangu. Nitamwelezea kila mmoja wa wahojiwa wangu katika mazingira yake ya kazi. Uandishi wangu unahitaji kumchukua msomaji; inahitaji kumfanya aone, asikie na ahisi mambo yote nayoyaona, kuyasikia na kuyahisi.

  1. Mwegemeo wa habari.

Nachokiona, kukisikia na kukihisi uwandani kinaniacha na wazo moja kuu: wakazi wa hapa wamechukizwa na mradi huu wa ujenzi wenye uchafuzi mkubwa, mazingira yao ya asili yameharibika kwa kiasi kikubwa sana tangia ujenzi kuanza. Ni kigongo (scoop), nilichopewa na Mwenda Ngamani, mwenyekiti wa chama cha wakazi wa kisiwani wasioridhishwa na ujenzi. Wakazi wa kisiwani hapo inasemekana wanaandaa maandamano kuonesha hasira yao. Huo ndiyo mwegemeo wangu wa habari! Natayari ninacho kichwa changu cha habari: “Kutafuta usalama Mark Mahela azua hofu kisiwani Sinde”…

  1. Ufunguzi mzuri.

Wazo zuri lililohuishwa kupitia wahusika thabiti na kusimuliwa kwa kutumia maneno yenye mvuto hutoa ripoti nzuri. Mwenda Ngamani alinipa kile nilichohitaji kwa ajili ya ufunguzi mzuri kwa maswali yangu. Yeye ndiye mwenyekiti wa chama cha wakazi wa kisiwani wasioridhishwa na ujenzi. Nitamtaja katika “intro”, kwa kuanza habari yangu na moja ya maelezo yake yenye uzito mkubwa: “maisha katika kisiwa chetu kidogo tulivu yageuka jinamizi”. Kisha nitaelezea wasifu wake kwa ufupi, kuanzisha kile kitarajiwacho, kabla ya kuongeza maelezo yake mengine kadri habari yangu inavyoendelea.

  1. Mtiririko mzuri wa simulizi.

Uandishi mzuri pia unahitaji mtiririko mzuri wa simulizi, unaomchukua msomaji kutoa kwenye ufunguzi mzuri hadi hitimisho zuri. Nitatumia maneno ya Mwenda Ngamani kama mtiririko wa simulizi yangu. Nitaendelea kuandika habari yangu kwa kubadilika-badilika kutoka nukuu, maelezo, wasifu mfupi, maelezo ya mashuhuda na uchambuzi wangu wa maisha kwenye kisiwa hiki kidogo na kizuri, kilichovurugwa vibaya kwa ujenzi wa makao makuu ya Benki ya Wafanyakazi.

  1. Hitimisho zuri.

Hakuna uandishi mzuri wa habari bila hitimisho zuri. Hitimisho langu, kwa simulizi ya ziara yangu kwa wakazi wa kisiwani wasioridhishwa na ujenzi, itaakisi ufunguzi wangu. Nitatumia maneno ya Mwenda Ngamani kama hitimisho la habari yangu: “Inakera sana: kisiwa chetu si ngome!”

HISTORIA ILIYO HAI NI KWA WAKATI HUU, KWA HIYO NAANDIKA KATIKA WAKATI ULIOPO.