Menu

21. Layout page

Mpangilio wa gazeti ni kama kuonesha bidhaa kwenye dirisha la duka. Kusudi hapa ni kuonesha habari. Kanuni ni sawa sawa na zile za utunzi katika sanaa za maonesho. Kila ukurasa wa gazeti lazima usanifiwe kana kwamba ni picha ya mchoro inayotakiwa kuwekwa kwenye fremu, ikiwa na maeneo ya pili ya msisitizo yaliyopangiliwa kuzunguka mada kuu. Lakini kazi ya mwisho lazima ipendeze, isomeke na kuvutia.

Ukurasa uliopangiliwa vizuri una mlingano unaotoa taswira ya urari na mpangilio mzuri kuanzia tu pale unapouona.

Mhariri msanifu si mpaka rangi lakini, zaidi ni kama mnakishaji wa ndani ya nyumba. Anatengeneza maajabu yake ndani ya pembe nne za umbo la ukurasa. Anafanya kazi muhimu ya kiufundi, akipanga habari ya kwanza na ya pili ili kutoa mwonekano bora zaidi.

HII INAMAANISHA KUWEKA URARI, KATIKA MAENEO MAWILI.

Urari wa jumla, kwenye ukurasa, kati ya maeneo yenye wino na meupe: kati ya maeneo meupe ya karatasi na maeneo yaliyochapwa kwa wino. Ikiwa eneo jeupe ni kubwa sana, hakuna mambo mengi ya kusoma. Kama kuna maeneo makubwa sana yenye wino, habari zitakuwa zimefinywa sana na hakuna mambo mengi ya kusoma. Uwiano wa rangi: 3/4 wino, 1/4 eneo jeupe. Uwiano mzuri: 2/3 wino, 1/3 eneo jeupe. Uwiano wa kisanii: 3/8 eneo jeupe, 5/8 wino.

Urari mahsusi, ndani ya eneo lililochapwa, kati ya habari kuu na zinazofuatia, kwa upande mmoja, na kati ya habari zinazofuatia kwa umuhimu, kwa upande mwingine. Msisitizo wa habari kuu haupaswi kupunguza umuhimu au kufunika habari nyingine.

Msanifu wa kurasa anatatua jambo hili kwa kuangalia:

  • kingo za ukurasa kuzunguka maeneo yaliyopigwa chapa,
  • idadi na unene wa safuwima kwenye ukurasa.
  • fonti zinazotumika kwenye habari,
  • ukubwa na upana wa kila herufi iliyotumika katika kila habari na kichwa cha habari,
  • urefu wa mistari,
  • nafasi kati ya maneno, mistari na safuwima.

Msanifu wa kurasa anatengeneza  mchoro wa awali kwa kutumia mifano ya mchoro. Ana idadi kubwa ya mifano hiyo, au anaweza kutengeneza mmoja mahsusi. Linapokuja suala la kusanifu kurasa, kuna mapokeo, mazoea, tabia, lakini hakuna kanuni za kudumu, mbali ya kutumia hekima na kutambua kitu kizuri.

KUONESHA HABARI KUU.

Jambo muhimu la kuzingatia kwa kila ukurasa, angazio lake, mkazo wake, ni habari yake kuu. Kila ukurasa una habari kuu moja tu. Inapewa kipaumbele: juu ya ukurasa. Ina kichwa cha habari kikubwa zaidi. Muundo wake, ukubwa wa kichwa chake cha habari na picha zozote zinazoendana nayo ndizo zinazotawala namna habari nyingine zitakavyowekwa kwenye ukurasa. Lakini msisitizo wa habari kuu haupaswi kupunguza umuhimu au kufunika habari nyingine, ambazo kila moja, pia ni muhimu sana. Msanifu wa kurasa hujitahidi kupata mpangilio ulio mzuri zaidi: Anazingatia uwiano na namna habari zitakavyokaa katika ukurasa.

KUTAFUTA UWIANO UNAOENDANA.

Elimu ya namna bora zaidi ya kuweka uwiano wa habari moja moja na kama kazi yote kwa jumla ni ya zamani kama ilivyo sanaa ya uchoraji au muziki. Sanaa ya usanifu wa kurasa inapata msukumo wake kutoka unadhifu wa uwiano unaotumika katika sanaa nyingine.

Unadhifu wa uchapaji unaepuka madhara ya mlingano kwa kutumia kanuni ya 4-2-1: ikiwa kichwa cha habari cha habari kuu kinachukua safuwima nne za ukurasa, kawaida ya utendaji inalazimu kusiwe na kichwa cha habari kingine kwenye ukurasa huo kinachochukua safuwima tatu, kwa vile hilo linaweza kuondoa kuonekana kwa habari kuu. Hata hivyo, kunaweza kuwa na vichwa vya habari kadhaa vya safuwima moja au mbili ndani ya ukurasa.

Unadhifu wa uchapaji huzuia mtawanyiko wa kuonekana kwa kutumia kanuni ya 6-3-2: ikiwa habari kuu ina kichwa cha habari kinachochukua safuwima sita juu ya ukurasa, utendaji wa kawaida unalazimu kuwe na habari moja tu kwenye ukurasa huo yenye kichwa cha habari kinachochukua safuwima tatu, na ikiwezekana iwe katikati au chini ya ukurasa, wakati pia kunaweza kuwa na habari kadhaa zenye vichwa vya habari za safuwima mbili katika ukurasa huo.

UWIANO WA DHAHABU.

Namna bora zaidi ya kupata unadhifu wa uwiano wakati wa kusanifu ni kugawa ukurasa katika maeneo manne kwa kutumia Uwiano wa Dhahabu uliotumika tangu zamani (kwa kugawanya maeneo ya ukubwa wa  1.618). Hilo linahakikisha kwamba maeneo ni “makubwa na uwiano wa wastani“, kunukuu maneno ya mtalaamu wa mahesabu wa Kiyunani, Euclid.

Hesabu yake ni rahisi, ukurasa uwe na ukubwa wowote ule (angalia nyongeza):

Gawanya upana (W) wa ukurasa kwa Uwiano wa Dhahabu:

Upana wa ukurasa ÷ 1.618 = x

Toa jibu kutoa kwenye upana (W):

Upana wa ukurasa – x = y

Pima thamani ya “y” kwenye upana juu ya mstatili (AB), ikiwezekana kwa kuanzia pembe ya juu kulia (B) ya mstatili.

Thamani hii ya “y” ndipo inaanzia kupima Pointi P1 kwenye upana (AB) wa mstatili.

Kwa kutumia Pointi P1, chora mstari wa wimakugawanya sehemu ambazo haziko sawa lakini katika  mgawanyo wa “Uwiano wa Dhahabu”.

fanya vivyo hivyo na urefu (H) wa ukurasa ili kuugawa ukurasa kimshazari kwenye Pointi P2, ikiwa imepimwa kutoka pembe (C) ya kulia ya mstatili.

Sasa ukurasa umegawanywa katika mistatili minne tofauti inayotengeneza mgawanyo nadhifu wa ukurasa wote unaoonesha usafi, ufasaha na uanuwai.

Kila moja ya maeneo haya manne bado yanaweza kugawanywa, kama itahitajika, kwa kutumia kanuni hiyo hiyo. Mchoro huu mkuu unaweza kurekebishwa kwa namna mbalimbali, wima au mshazari, kuepuka vichwa vya habari kuteremka kama “ngazi” kwenye ukurasa na kuepuka kugonganisha vichwa vya habari kwa habari zinazowekwa katika maeneo yanayorandana kwenye ukurasa.

KUMBUKA:

  • Chagua fonti kwa umakiniTumia mtindo rahisi: tofauti kubwa sana ya fonti za uchapaji itamchosha msomaji. Tumia fonti mbili tu: fonti ya “serif”, kama vile Times, kwa habari, na fonti ya “sans-serif”, kama vile Helvetica, kwa vichwa vya habari na vichwa vya habari vidogo. Cheza na fonti za “roman”, iliyokolezwa wino na ya mlazo kutegemea na aina uandishi wako.
  • Kuwa makini na aya yako ya kwanzaAya yako ya kwanza si mwanzo wa habari yako. Ni utangulizi mfupi wa kutambulisha habari yako na kumfanya msomaji aendelee kusoma.
  • Zingatia ni sehemu gani unapokatia habari yakoHuwezi kukata habari yako mahali popote, na hasa si katikati ya sentensi, hata kwa ukurasa wa mbele, ikiwa habari yako inaendelea katika kurasa kadhaa ndani ya gazeti. Usiruhusu ukataji wa habari ukafanya usomaji kuwa mgumu na usio na mtiririko.

Timu za chumba cha habari ambazo zinaweza kuandaa mipango na kuizingatia zina uwezo mkubwa wa kuandaa usanifu wa mifano yao moja kwa moja na kuzipeleka kwa wahariri wasanifu kwa masahihisho na uchapaji.