Menu

11. “reli”

Kwa waandishi wa habari wa magazeti, usanifu ni kama mchezo wa kuelimisha. Ni mchoro kwenye karatasi au kwa sasa zaidi kwa kompyuta unaoonesha mwonekano wa ukurasa mmoja mmoja wa gazeti ukavyokuwa baada ya kuchapwa. Muhtasari huu ni mwonekano wa awali wa namna ambavyo habari itapangwa na kupewa kipaumbele kutokea ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho.

KANUNI KUU

Si kurasa zote za gazeti zina mvuto sawa kimwonekano.

Ukurasa wa kulia kiasili unaonekana kirahisi zaidi kwa msomaji, wakati msomaji lazima afungue gazeti kuona ukurasa wa kushoto.

Habari za kurasa za namba witiri mara nyingi huonekana zaidi kuliko habari za kurasa za namba shufwa.

Kurasa zenye mvuto mkubwa zaidi, bila shaka, ni ukurasa wa mbele, ambao ndiyo ukaribisho kwenye gazeti, pamoja na kurasa nambari 3, 5, 7, nk. kwa sehemu kubwa hizi zinachukuliwa ni kurasanyetiza gazeti, yaani zile zinazotumiwa kutoa habari za hivi punde.

Kinyume chake, kurasa za nambari shufwa, yaani 2, 4, 6, 8, nk. hutumika zaidi kuandika habari kuu zinazoendelea ndani na habari za pili kwa umuhimu. Zinaunda kile kiitwacho kurasa “baridikatika gazeti, yaani zile zinazotumika kuchapisha habari zisizo muhimu sana.

Maeneo mengine mawili katika gazeti yanayomvutia zaidi msomaji: kurasa mbili za kati na ukurasa wa nyuma.

Kurasa mbili za kati ni sehemu bora zaidi ya kuchapisha makala ndefu. Zinatengwa kwa habari za kina, habari za uchunguzi, makala, wasifu na mahojiano ya kina.

Ukurasa wa nyuma, ambao mara nyingi ndiyo wa mwisho kukamilika, kwa kawaida huandika habari za mwishoni mwishoni kupokelewa. Kama ilivyo kwa ukurasa wa mbele, ni chaguo zuri pia la kuangazia maoni na vibonzo.

KUPANGILIA HABARI

Kutofautisha kati ya kurasa za “motomoto” na “baridi” si tu utaratibu wa msingi wa kushughulikia habari kulingana na “joto” lake. Inawezesha pia uandikaji habari kutekelezwa vyema siku nzima kuepuka msongamano dakika za mwisho. Habari nyingi zinaweza kuandika kabla na kusanifiwa saa chache kabla ya kuchapwa ikiwa kutakuwa na mpangilio mzuri wa kazi na ratiba kuzingatiwa. Habari hizo zinaweza kujumuisha zile zinazochapishwa kurasa za kati, habari zinazoweza kuchapishwa wakati wowote, habari za mfumo wa jarida au habari za pili kwa umuhimu zinazowekwa kwenye kurasa za nambari shufwa. Uzalishaji unaopangiliwa vizuri utahakikisha gazeti lenye ubora zaidi.

KIOLEZO CHA MSINGI

Usanifu wa gazeti dogo mahalia kwa kawaida huhusisha kurasa 12. Idadi hii ya kurasa inaweza kubadilishwa kirahisi na kuongezeka maradufu (kurasa 24) kwa gazeti kubwa mahalia la kila siku, kuongezeka mara tatu (kurasa 36) kwa gazeti la kikanda la kila siku au kuongezeka mara nne (kurasa 48) kwa gazeti la kitaifa la kila siku. Kila kazi ya usanifu inagawanywa kulingana na habari na mgawanyo wa kazi. Ina kurasa nyingi kwa ajili ya habari motomoto na zile za baridi kuwezesha kuandika habari zaidi za mambo yanayotokea hivi punde.

Gazeti dogo mahalia la kila siku

  • Ukurasa wa mbele: habari kuu: kichwa cha habari (“Kigogo wa Benki Mark Mahela atekwa”), kivutio cha habari (aya ya kwanza ambayo ni muhtasari wa habari, kumwelekeza msomaji kilichopo ndani ya gazeti + picha au kibonzo).
  • Ukurasa wa 2: habari zilizohaririwa mapema zikilenga “habari zenye manufaa”, kama vile “barua za wasomaji”, kwa mfano.
  • Ukurasa wa 3: mwendelezo wa habari kuu lakini ikiwa na kichwa cha habari tofauti: “Utekaji wa wafanyabiashara waongezeka”… Na kichwa kidogo cha habari: “Mkuu wa Polisi aelezea wimbi hili” (ukurasa wa habari motomoto).
  • Ukurasa wa 4: Maisha ya mtaani (ukurasa wa habari baridi).
  • Ukurasa wa 5: Maisha ya mtaani (ukurasa wa habari motomoto).
  • Ukurasa wa 6-7, kurasa mbili za kati:habari mahalia, makala au habari ya uchunguzi (ukurasa wa habari baridi).
  • Ukurasa wa 8: Biashara (ukurasa wa habari motomoto).
  • Ukurasa wa 9:Utamaduni (ukurasa wa habari baridi).
  • Ukurasa wa 10: Michezo (ukurasa wa habari motomoto).
  • Ukurasa wa 11: Habari zinazogusa jamii (ukurasa wa habari motomoto).
  • Ukurasa wa 12: Wasifu wa kila siku (habari baridi), safuwima fupi kwa ajili zinazoletwa mwisho mwisho (habari motomoto).

 ***

Kiolezo cha usanifu kinachotumika kwa gazeti la kitaifa la kila siku (robo tatu ya kursa za habari baridi)

  • Ukurasa wa mbele: kivutio cha kusoma habari za kwenye gazeti.
  • Ukurasa wa 2: habari zinazogusa jamii.
  • Ukurasa wa 3: mwendeleo wa habari za ukurasa wa mbele.
  • Kurasa za 4, 5, 6: mambo ya nje (ikiwemo kurasa mbili za habari baridi).
  • Kurasa za 7, 8, 9: mambo ya ndani (ikiwemo ukurasa mmoja wa habari baridi).
  • Kurasa za 10, 11: jamii (ikiwemo ukurasa mmoja wa habari baridi).
  • Kurasa za 12, 13: kurasa mbili za kati.
  • Kurasa za 14, 15: biashara na jamii.
  • Kurasa za 16, 17: utamaduni (ikiwemo ukurasa mmoja wa habari baridi).
  • Kurasa za 18, 19: michezo (ikiwemo ukurasa mmoja wa habari baridi).
  • Kurasa za 20, 21, 22: habari zenye manufaa (ikiwemo kurasa mbili za habari baridi).
  • Ukurasa wa 23: burudani, programu za runinga na redio, michezo.
  • Ukurasa wa24: habari zinazoletwa mwishoni mwishoni.

“HABARI ZA MWANZO MWANZO”

Kurekebisha usanifu inakuwa rahisi zaidi kutokana na kazi ya waandishi wa habari wa kwanza kuingia kazini katika kila idara au kitengo, ambao wanachaguliwa kwa zamu. Jukumu lao ni kugawa kazi kwa kila mwanatimu. Wanaangalia habari kutoka mashirika ya habari na habari kutoka mtandaoni na kupokea taarifa rasmi kwa vyombo vya habari na barua za wasomaji. Jambo hili linaokoa muda wa kila mmoja na kuboresha usanifu wa gazeti.