Menu

16. GP na wataalam

Mazingira ya uandishi wa habari yanahitaji waandishi wa habari kuwa watu wasio na ubobezi wowote. Zaidi ya yote, habari huhusu kila mada unayoweza kuifikiria na waandishi wa habari lazima waifanye kazi hiyo. Lakini wakiandika kutoka mada moja hadi nyingine, wanakuwa katika hatari ya kuandika mambo yasiyo sahihi. Kwa hakika, moja ya mambo ambayo mara nyingi waandishi wa habari hukosolewa kwayo, ni kwamba wanaongea kwa sababu tu ya kuongea. Lakini kuwa mtu asiye na ubobezi haimaanishi kuwa mtu asiyefahamu mambo au asiye na uelewa wa kina. Wataalamu wazuri nao ni watu wanaofahamu mambo mengi kwa juu juu tu lakini wanaopenda kufanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa sana.

KUKUZA UHODARI

Kwa tafsiri yake, uandishi wa habari unashughulika na kila habari unayoweza kuifikiria. Waandishi wa habari hawachagui nini waandike; habari ndiyo huwachaguliwa nini wakiandike. Kwa hiyo, kazi yao huwataka kuwa na ujuzi mwingi, kama si kujua kila kitu. Popote pale walipo, lazima waoneshe ujuzi wako kwa kiwango kile kile, ikiwa ni kwenye ofisi ndogo au maeneo makubwa. Mwandishi wa habari mzuri, kama ilivyo kwa Daktari wa Kawaida mzuri, anapaswa kushughulikia kwa umakini mambo madogo sawa na atakavyoshughulikia mambo makubwa. Ikiwa wewe ni mwandishi mdogo au mwandishi maalum maarufu, uandishi wa habari unataka unyenyekevu na kuwa tayari kufanya kazi.

Ni suala la akili yako kukubaliana nalo:

* Kuandika habari ndogo kabisa kana kwamba ni habari kubwa: kwa  umakiniule ule.

* Kuandika habari ya kawaida kana kwamba ni moja ya habari zenye umuhimu mkubwa: kwa usahihi ule ule.

Kuandaa mahojiano mafupi ya sauti ya watu kwa namna ile ile kama mahojiano makubwa : kwa kutumia “mwongozo wa mahojiano”.

* Kuichukulia kila ripoti kana kwamba ni habari nzuri ya kusimulia.

* Kuona fursa ya taswira  nzuri kwa kila mtu unayekutana naye.

* Kuona fursa ya habari ya kipekee katika dondoo ndogo kabisa.

* Wakati wowote ule jambo lolote lisilokuwa la kawaida hata liwe dogo vipilinapotokea, kujiuliza kunaweza kuwa na kitu cha kuchunguza hapa?

Kutoa kipaumbele na kupangilia habari mahalia kwa umakini ule ule wa habari za kitaifa: kwa kuwajibika wakati wa kuandika habari. Kinachotokea ndani kwangu ni muhimu zaidi kuliko kinachotokea mtaani. Kinachotokea mtaani kwangu ni muhimu zaidi kuliko kinachotokea wilayani. Kinachotokea wilayani kwangu ni muhimu zaidi kuliko kinachotokea jijini. Kinachotokea jijini kwangu ni muhimu zaidi kuliko kinachotokea nchini. Kinachotokea nchini kwangu ni muhimu zaidi kuliko kinachotokea katika kanda, nk.

NI SUALA LA KUZOESHA AKILI YAKO:

* Ikiwa habari inachelewa kueleweka, chukua hatua! Naanzisha mazungumzo kwa kuwasiliana na wasomaji; barua na maoni yao ni mgodi wa dhahabu pale napokuwa sina habari ya kuandika. Nahitaji kujiongeza tu kuhusu uwezekano wa kuwa na habari kwa kutumia michango ya wasomaji wanaofuatilia suala hilo.

* Ikiwa kwa kiasi fulani habari ni ya kawaida tu, kuwa mbunifu! Natafuta miegemeo ya habari isiyotegemewa kwa ajili ya kuandika habari za kawaida. Nahitaji tu kuangalia chochote kile ambacho si cha kawaida na kuchagua aina isiyo ya kawaida ya uandishi kwa ajili ya kuandika habari ya kila siku.

* Ikiwa habari haina mvuto, naingia kazini! Naibua maelezo thabiti ya mashuhuda kunogesha habari inayosimuliwa kila siku. Nahitaji tu kuongeza vyanzo vipya muhimu vya habari kwenye shajara yangu kila siku ili kwmaba niweze kuandika kuhusu habari yoyote ile papo hapo, lakini kila mara kwa weledi.

* Ikiwa habari haihamasishi, naboresha aina yangu ya uandishi! Naandika habari fupi ya kupendeza, inayoundwa na sentensi moja iliyoandikwa vizuri, kwa kutumia habari ndogo kutoka mashirika ya habari. Ningeweza hata kuandika maoni mapya kila siku kwa kutumia habari fupi za kuburudisha…

JITAHIDI KUWA MAHIRI

Huwezi kuwa mbobezi bila kufanya kazi. Kuna baadhi ya mada ambazo huwezi kuziandika vizuri kama huna elimu husika ya kukusaidia kuzichambua kwa kina. Huwezi kuelezea upelelezi wa polisi kwa ufasaha unaotakikana ikiwa hufahamu lugha ya mwenendo wa kisheria. Huwezi kuchambua kwa usahihi hali ya kifedha ya kampuni fulani ikiwa huelewi tofauti kati ya mauzo na gharama za uendeshaji. Huwezi kukosoa kazi ya sanaa kiweledi ikiwa mwenyewe huna viwango vya kisanii.

Ni suala la kujiendeleza binafsi.

Magazeti bora ni yale yenye waandishi wa habari ambao ni wataalamu kutokana na habari zao kuwa na manufaa katika mada zote: kuanzia ngumu kabisa (elimu, mahakama, polisi, sayansi, afya, utamaduni, dini, masuala ya kijeshi, nk.) hadi habari za kila siku (siasa za ndani, siasa za kimataifa, uchumi, masuala ya kijamii, michezo, nk.).

Mwandishi yeyote asiye mbobezi anaweza kuwa mbobezi katika nyanja yoyote ikiwa atataka na kujitahidi kufanya  kazi ya ziada ambayo jambo hili linahitaji. Si suala la kurudi shule, unahitaji tu kutenga muda wa kujifunza.

* Jiwekee lengo la kuwa bora katika eneo ulilolichagua au eneo ambalo limeangukia mikononi mwako kutokana na aina ya kazi unayofanya.

* Jitengee muda wa kujisomea, ukitafuta kupata ushauri kutoka kwa waandishi wa habari waandamizi.

Soma kila kitu kinachosemwa na kuandikwa kuhusu mada husika, hususani, chochote kilichoandikwa na magazeti mengine.

* Jifunze, kama ulivyosoma shule, ukitumia zana zote muhimu ili uweze kuwa gwiji wa eneo lako: sheria, kanuni rasmi, miongozo ya kiweledi, nk.

* Kuza mtandao wa vyanzo vyako binafsi vya habari katika eneo husika ambavyo vinaweza kuthibitisha uelewa wako endapo utakuwa na shaka.

* Hudhuria wewe mwenyewe, mara nyingi kadri iwezekanavyo katika sehemu (mikutano, mikusanyiko, vikao, nk.) ambapo wataalamu wanakutana kujadili mambo, hata kama wakati mwingine itakuwa ni kupoteza muda.

* Epuka kutumia lugha inayotumiwa na kundi fulani la wasomi wakati unapoandika kuhakikisha unaeleweka na jamii lakini pia uwe sahihi kiasi cha kwamba wabobezi waithamini kazi yako.

Timu zenye ufanisi mkubwa sana katika uandishi wa habari ni zile zinazoweka ushirikiano kati ya waandishi wasio na ubobezi na waandishi wabobezi na kufanya hilo kuwa kanuni ya kawaida.