SI PICHA ZOTE HUHABARISHA KWA NAMNA INAYOFANANA
Kuna picha zinazotoa maelezo. Hizo ni picha za kawaida au mtizamo, kama ville picha za mandhari, au matukio ya shughuli za binadamu kwa kutokea mbali. Ile hali yake ya kutoa tu mwonekano ina maana kwamba picha hizo zina ongezeko dogo sana la thamani. Kwa ujumla thamani yake ya kihabari ni mbaya. Isipokuwa pale mazingira ya wakati zinapopigwa – na mlengo uliotumika kupiga picha – unazipa thamani ya kikumbukumbu.
Kuna picha zinazotoa simulizi. Hizi ni picha za kati, picha za Kimarekani, picha zilizopigwa kwa karibu, kama vile picha ziliopigwa kwa karibu na matukio ya shughuli za watu, picha za maumbo katika ukubwa wake wote, picha zinazooneka kuanzia juu ya magotini hadi kiunoni au kuanzia kiunoni hadi kifuani. Thamani yake ya kutoa simulizi ina maana kwamba picha kama hizo zina ongezeko kubwa la thamani.
Kuna picha zinaleta mshtuko. Hizi ni picha zilizopigwa kwa karibu na karibu sana, kama vile sura inayoonekana kwa karibu sana au mwonekano wote wa picha iliyopigwa kwa karibu sana. Matokeo yake ya kihisia yana maana kwamba picha kama hizo zina ongezeko kubwa sana la thamani.
Picha ni kipande cha maisha yanavyoonekana wakati huo huo, na jambo la muhimu kuhusu picha ni namna inavyopigwa. Picha mgando kuhusu maisha hazina nafasi katika gazeti la kila siku. Picha zote lazima zioneshe uhai. Ingawa yeye si mpiga picha, mwandishi wa habari anahakikisha kwamba picha zinazotarajiwa kutumika katika habari yake zinaonesha matukio ya uhai na zimepigwa kwa namna ambayo bila ya kujali jambo kuu litakalofafanuliwa, mara zote zitakuwa na uhai, iwe ni mbele au kwa nyuma.
Nitaongeza picha ya mwonekano mpana zaidi wa habari yangu ya kuwasili kwa Mark Mahela kwenye bandari ya kisiwa cha Sinde na timu yake nzima ya ulinzi. Kwa hiyo wasomaji wangu wataona umuhimu wa mradi huo kwa benki mashuhuri ya Wafanyakazi.
Ripoti yangu kuhusu wakazi wa kisiwani wasiofurahishwa na mradi itafafanuliwa na matukio kadhaa ya maisha ya kila siku ambayo yataonesha picha zilizopigwa kwa umbali wa kati, wanaume, wanawake na watoto wakijiandaa kufanya maandamano dhidi ya makazi yenye ulinzi wa hali wa juu ya Mark Mahela.
Picha yangu ya Mwenda Ngamani itaonesha picha iliyopigwa kwa karibu ya mwenyekiti huyo wa chama cha wakazi wa kisiwani wasiofurahishwa na ujenzi akitabasamu kati ya matangazo na mabango anayoyaandaa kwa ajili ya maandamano.
Mahojiano yangu na Mark Mahela yatanogeshwa na picha iliyopigwa kwa karibu sana ya sura inayoonesha dhamira ya mmiliki huyo mashuhuri wa benki.
Kisha nitaandika maelezo ya picha ambazo mimi na mpiga picha wangu tutazichagua kwa ajili ya kuzichapisha kwenye kurasa mbili za kati kuhusu matukio yanayoendelea hapo kisiwani kwa ajili ya toleo la mwishoni mwa wiki. Zitakuwa ni mkusanyiko wa picha zilizopigwa kwa karibu na zitakuwa na kichwa cha habari kisemacho: “Mark Mahela, kuwasili kwake.” Mchango wangu kama mwandishi utakuwa umekomea kwenye kuandika maelezo ya picha na sura ya maoni ya jumla…
Kama nina waraka au picha yenye thamani kubwa sana kimaelezo, nitaomba ichapishwe ukurasa mzima.
VIBONZO VYA MAGAZETINI NI ENEO LA UHURU WOTE
Vibonzo vya magazetini ni muhimu sana! Hakuna mtu anayevichezea! Unapokuwa na mchora vibonzo au vibweka ambaye anaweza kuweka habari katika muhtasari wa michoro michache, na kuiandikia bila kuegemea upande wowote, wakati mwingine akitabasamu na wakati mwingine akinuna, unatokea kuamini mvuto wake. Unafurahia kujadili michoro yake. Kanuni nzuri ya kawaida ni kumuomba mchora vibinzo wako awasilishe michoro mitatu (angalau miwli) kuhusu habari kwenda kwa mhariri mkuu kila siku. Uamuzi wa mchoro upi utumike unafikiwa kwa maridhiano, lakini kauli ya mwisho ni ya mhariri mkuu.
HABARI KWA NJIA YA MICHORO SI KWA AJILI YA UDUNI
Utajiri wa habari kwa njia ya michoro huipa habari thamani ya rejea, ilimradi tu kwamba maudhui yake yenyewe yako sahihi. Waandishi wa habari hawaruhusiwi kufanya makosa wanapochapisha grafu, kielelezo, au ramani sambamba na habari yao. Kosa dogo tu katika maelezo hutia doa kazi yao yote. Kuhabarisha watu kwa kupitia habari kwa njia ya michoro ina maana kuweka mkazo wa kisayansi katika kuandika habari. Hii huhitaji kufikiria, matumizi na kuratibu kilichopo wakati wa vikao vya habari.
Ramani hutoa taswira halisi. Nahitaji kutumia ramani ndogo kuwaonesha wasomaji wangu kwa haraka ofisi za Benki ya Wafanyakazi duniani kote, ambayo nitatumia mishale kuonesha uwekezaji na kujiondoa kulikofanyika hivi karibuni.
Graphu zinaelezea. Nina takwimu halisi kuhusu mwenendo wa bei za soko la hisa tangu kuhamishiwa makao makuu ya Benki ya Wafanyakazi kwenye kisiwa cha Sinde; mpindo kwenye grafu utalielezea hilo vizuri zaidi kuliko uchambuzi…
Vielelezo hufafanua. Ugharamiaji wa ujenzi wa makao makuu ya Benki ya Wafanyakazi kisiwani Sinde unahusisha makampuni mengi ya mfukoni; kielelezo kuhusu utaratibu huu utaeleza kwa ubayana zaidi kuliko kutumia maelezo magumu.