SIRI KUMI ZA MAHOJIANO MAZURI:
- Jenga mazingira ya uaminifu
Mahojiano ni sawa na mechi ya mchezo. Mhojaji siku zote huanza katika hali ya unyonge kwa sababu ndiye anayeomba kupata jambo fulani. Ili kuufanya mchezo huu kuwa wa kirafiki, mhojiwa hapana budi kuanza naye kwa tahadhari. Kuwaandikia kutawafanya wajisikie amani zaidi kuliko kuwapigia simu. Ni muhimu kumthibitishia mhojiwa wako kwamba maelezo yake kama shuhuda yana thamani kubwa na unamuhakikishaia kwamba hakuna chochote asemacho kitakachochapishwa bila ridhaa yake. Pale napomwandikia Mark Mahela ili kupata mwitikio wake kwa ugunduzi wangu kuhusu kujenga makao makuu ya Benki ya Wafanyakazi katika eneo la hifadhi ya uoto wa asili, najaribu kumshawishi. Nawekea mkazo ukweli kwamba, kama mhojaji, nampa fursa ya kujibu malalamiko kuhusu mbinu zake ambayo yameenea kisiwani…
- Hakikisha kwamba unakuwa juu
Mahojiano na viongozi wa kisiasa, watumishi wa umma, wakurugenzi wa makampuni na waandishi hayafanani. Lakini bila kujali unamhoji nani, mahojiano yanaweza tu kuzaa matunda ikiwa umejiandaa vyema. Naomba mahojiano na Mark Mahela pale napojisikia niko tayari kukabiliana naye. Najisikia niko tayari napokuwa nimekusanya nyaraka za kutosha kumhusu, rafiki zake, adui zake, na napokuwa na “mwongozo imara wa kufanya mahojiano”, yaani orodha ya maswali ya kina na sahihi kiasi cha kukanusa mbinu zake za kunitoa nje ya lengo na kumkabili kisawasawa…
- Chagua mkakati sahihi
Kuna aina tatu za mahojiano, ambazo zote zinatoa matokeo tofauti.
* Mahojiano yenye maswali ya mpangilio hujumisha uulizaji wa maswali mahsusi sana na kukataa kutoka nje ya mstari na majibu ya kukwepa maswali. Ni mbinu ya kimapambano, inayofaa zaidi katika mahojiano mafupi kama vile “sauti ya umma” yanayobwagizwa katikati ya taarifa kuu: maswali matatu, kila moja ikiwa na majibu ya mistari mitatu hadi mitano… Hatutamuhoji mmiliki mashuhuri wetu wa benki kwa kutumia mtindo wa “sauti ya umma”!
* Mahojiano ya maswali yasiyo na mpangilio hujumuisha kuuliza swali la wazi na kisha kumwacha mhojiwa alijibu apendavyo. Mbinu hii ya mahojiano ya kirahisi inafaa kwa kutafuta kuelewa hulka ya mhojiwa pale unapokuwa hujui mengi kumhusu, lakini mara nyingi haitoi maelezo yoyote. Ikiwa nitamwacha tu Mark Mahela azungumze ni dhahiri hataniambia ni namna gani alipata kibali cha kujenga jengo lake lenye ulinzi mkali katika eneo la hifadhi ya uoto wa asili.
* Mahojiano ya maswali yenye mpangilio kiasi ndiyo inafaa zaidi katika uandishi wa habari. Inahusisha utumiaji wa maswali ya kuhama kutoka ya wazi kwenda yale yanayombana mtu, ya jumla na ya kina. Mbinu hii ya kutumia maswali ya kuhama, hukuwezesha kuuliza upya maswali, kukuza mazungumzo, kutengeneza mazingira ya kubadilishana taarifa au hata kushirikiana. Nitatumia mbinu hii ya kujumuisha mambo yote kwa mahojiano yangu na Mark Mahela. Nitaanza na maswali ya jumla sana: “Kwa nini uliamua kuhamisha makao makuu ya Benki ya Wafanyakazi kwenda kisiwa cha Sinde?” Nitamwacha aongee kwa uhuru kwa muda. Sitamkatisha. Kwa kusikiliza kwa umakini na kutabasamu, nitamfanya ajisikie amani. Kisha, wakati anaongea, nitamkatisha kwa upole kwa kuuliza maswali mahsusi kwa kumpa rejea kuthibitisha uwezo wangu: “Nilikuwa Sinde wiki iliyopita, nilipata kifungua kinywa na Maafisa wa Shirika la Taifa la Maeneo ya Hifadhi na niliambiwa kwamba ulinufaika na idhini ya upendeleo ya kujenga kisiwani hapo… Hiyo ni kweli?”
- Chagua sehemu sahihi
Huwezi kuwahoji watu mahali popote tu. Huwezi kumhoji Mark Mahela kwenye baa ya mtaani. Kama mhojaji, inabidi umfuate. Epuka maeneo ya umma, hasa baa na migahawa. Kelele za mahali hapo zinaondoa uwepo na uwepo wa watu wengine wakishuhuda mazungumzo unaweza kumkosesha amani mhojiwa wako. Chagua mahali kimya na tulivu, hasa ofisini au sebuleni. Maeneo ya umma yanaweza kufaa pale mnapokuwa na mazungumzo yasiyo rasmi na mashuhuda wa ziada au watoa taarifa, ambao hawawezi kutambuliwa na jamii.
- Chagua kauli sahihi
Mahojiano yanaweza kuwa sawa na mchezo, lakini si pambano la masumbwi. Ni kikao tata cha ana kwa ana, lakini kile ambacho kila upande unajaribu kumvuta mwenziwe. Mhojaji kutumia nguvu inaweza kutofanikisha lengo. Ukali hautampa sababu mhojiwa wako kukupa siri zake. Mhojiwa si adui yako. Haina maana ya kuchikoza, kugombana au hata kumshinda. Inahusu kutengeneza mazingira ya kuheshimiana wakati ule mazungumzo yanapofanyika. Kauli sahihi haijigambi, inavumilia na inakaribisha. Si lazima kwamba nakubaliana na Mark Mahela, lakini natambua haki yake ya kujieleza kwa uhuru na, kama nikiona ipo haja ya kukanusha, nafanya hivyo kwa heshima.
- Fahamu jinsi ya kuuliza maswali yako
Maswali ya chuki, utatanishi au yasiyohusika na mada hayatamfanya mhojiwa wako kuwa na amani. Namna sahihi ya kufanya mahojiano inahusisha maswali ya wazi, na sahihi, ambayo kila neno limepimwa, kwa mtiririko unaoenda kwa mpangilio wenye mantiki kuhusu jambo kuu, na ambayo yanamuonesha mhojiwa, kupitia kutolegalega na usahihi, kwamba una uelewa mzuri wa jambo husika au suala mnalojadili. Hii ndiyo sababu “mwongozo wako wa mahojiano” ni muhimu sana. Kuandaa mwongozo huu kabla ya mahojiano yako hukuwezesha kumiliki mahojiano hata kama mhojiwa wako ana tabia ya kukwepa maswali…Ikiwa nitamuuliza Mark Mahela kuhusu uwekezaji kwenye jengo hili lenye ulinzi mkali inamaanisha nini, nahitaji kuwa na vigezo thabiti vya mlinganisho, kwa mfano gharama halisi za ujenzi wa jengo la kisasa ambalo mshindani wake, mmiliki wa benki Bintu Bingi, alilolijenga hivi karibuni, vinginevyo mhojiwa wangu hataniona kuwa ni mtu makini.
- Uliza maswali sahihi
Swali zuri, ni la wazi, sahihi, linaloeleweka, liliso na mwegemeo fulani na linaloulizwa kwa namna isiyomfanya mhojiwa kukupa jibu unalolitaka, lakini lenye maana kiasi kwamba jibu linampa mhojaji maelezo ya karibu sana kile anachokitafuta kutoka kwa mhojiwa. Hilo linaweza kuwa swali la nyongeza. Kuuliza swali sahihi la nyongeza kwa wakati sahihi huhitaji ufahamu wa kina wa mada yako. Mhojaji hufanikiwa katika hilo kupitia mwendelezo wa maswali yake, kuanzia rahisi na kuishia na maswali ya nyongeza magumu. Nitakuwa na swali zuri la nyongeza la kumuuliza Mark Mahela pale atakapothibitisha kwamba alinufaika na idhini ya upendeleo iliyomwezesha kujenga kisiwani Sinde: “Ujenzi wa makao makuu mapya haya unahusisha uwekezaji mkubwa kwa Benki ya Wafanyakazi. Hali ikoje kwa upande wa wafanyakazi wako? Je, kupunguza wafanyakazi kulikotangazwa muda mfupi kabla ya kutekwa bado utaendelea?”
- Usijizuie wewe mwenyewe
Wakati mwingine maswali sahihi husababisha kukwepa swali au kukataa kujibu. Lakini usilegeze kamba. Wewe ni “mtafutaji ukweli” na kwa hiyo ni wajibu wako kuuliza tena, kwa upole, utulivu, lakini kwa ufasaha, angalau mara moja tena. Ikiwa hutapata matokeo bora, kukataa kwa mhojiwa inakuwa ni ukweli mkubwa, ambao unastahili kuripotiwa kwa wasomaji wako. Nategemea kwamba Mark Mahela hatajibu swali langu la nyongeza. Ikiwa atasema alitaka kusitisha mpango wa kupunguza wafanyakazi, hapana wanahisa wa Benki watamwachisha kazi kwenye mkutano mkuu wa wanahisa wa mwaka unaofuata. Lakini akikataa kujibu, nitaliweka hilo kwenye habari yangu…
- Andika maelezo ya mahojiano, lakini usipindishe ukweli
Kurekodi mahojiano ina maana kwamba mhojaji haitaji kuchukua maelezo mfululizo na humpa mhojiwa hakikisho kwamba maneno yao hayatabadilishwa. Lakini unaweza kurekodi tu kwa ridhaa ya mhojiwa, na lazima ukubali kuacha kurekodi ikiwa mhojiwa atataka hivyo. Pia unapaswa kusitisha kurekodi wewe mwenyewe, kwa heshima, ikiwa kutakuwa na kuingiliwa hata kidogo tu kwa mahojiano yenu, kama vile kupigiwa simu. Kurekodi haina maana kwamba huhitaji kuchukua maelezo. Kadri mazungumzo yanavyoendelea, andika hususani yale mambo ambayo hayatatokea katika rekodi: tabasamu, mshangao, kusita, ishara ya usoni, nk. Mwishoni mwa mahojiano, jadilianeni iwapo maelezo yoyote yanahitaji kufutwa wakati wa kuyaweka katika maandishi.
- Hitimisha kwa ufasaha
Hata kama vigezo vyote vimekubaliwa kabla, mwisho wa mahojiano pia ndiyo wakati wa mhojaji kumhakikishia mhojiwa jinsi maneno yake yatakavyotumiwa, ili kuepuka kutoelewana: chapisho kamili kama safu ya maswali na majibu, sehemu ya chapisho kama maelezo huru au maelezo yaliyochaguliwa kwa maafikiano, chapisho lenye haki ya kuoneshwa kwanza kile kitakachochapishwa, nk. Hilo ni chaguo la mhojaji, ilimradi amekuwa wazi kabisa na mhojiwa. Makubaliano yangu binafsi na Mark Mahela, kama kawaida, yatakuwa wazi kabisa: ataniruhusu kurekodi kila kitu anachokisema na kuchapisha maneno yake kama nipendavyo… lakini atakuwa na haki ya kukanusha. Ni kauli yake dhidi ya kauli yangu, inaonekana kuwa makubaliano ya haki.