Menu

09. Vyanzo

Ili kuwahabarisha wasomaji wako kwa usahihi, lazima wewe mwenyewe uwe na uelewa wa kile unachokisema. Mwandishi wa habari anahitaji vyanzo vya kuaminika kumsaidia kutenganisha ukweli na uongo, na kusambaza habari za ukweli. Hata hivyo, matumizi sahihi ya vyanzo vya habari yanataka kuchukua tahadhari na utaratibu unaofanana na ule wa kukusaidia kubaini ukweli.

KUNA AINA NNE ZA VYANZO VYA HABARI:

  1. Vyanzo vya habari vya kitaasisi. Hivi ni vyanzo vyote vya habari vya wenye mamlaka ya nchi: serikali, wizara, tawala, nk. Wanao upendeleo wa kuwa taasisi rasmi na mfumo na wanatoa habari rasmi. Ni muhimu kwamba shajara ya mwandishi wa habari iwe na maelezo binafsi ya wasemaji wote walioidhinishwa kwa niaba ya mamlaka hizo (msemaji, afisa habari, nk.). Andaa orodha na wasiliana nao mara tu wanaposhika nyadhifa zao, wakati bado wanaona ni heshima kwao kutambuliwa na vyombo vya habari (simu za kiganjani, anwani binafsi, nk.).
  2. Vyanzo vya habari vya kati.Hivi ni vyanzo vyote vya habari vyenye uhalali wa kijamii: vyama, vyama vya kitaaluma, vyama vya siasa, vyama vya wafanyakazi, nk. Vina upendeleo wa mara nyingi kufanya kazi kama kundi la mawazo mbadala linalotoa habari zisizo rasmi. Ikiwa mwandishi wa habari atachukua muda wa kujenga uhusiano mzurina washirika hawa wa kijadi, atanufaika kwa kupata habari ya ziada na mwanga muhimu sana wa jambo husika. Andaa orodha ya wasemaji tarajiwa na jenga urafiki nao kwa minajiri ya “kuwa nao karibu”.

KANUNI ILIYO FANISI: KUPEWA KITAMBULISHO

Katika kushirikiana na vyanzo vya habari vya kitaasisi na vya kati, ni kwa manufaa ya mwandishi wa habari mwenyewe kufafanua kazi yake. Kwa upande wa vyanzo vya habari vya kitaasisi, waandishi wa habari wanaweza kuomba kupewa vitambulisho wao wenyewe au wenzao. Mamlaka zote za serikali na mashirika ya kijamii hupendelea kuwa na waandishi wa habari wanaofahamika katika kushirikiana na vyombo vya habari. Kushirikiana kwa namna hii kwa pande mbili huhamasisha kuwepo mawasiliano ya kila siku.

Mfano wa barua ya kuomba kupewa kitambulisho: “Mheshimiwa Waziri, ninayo furaha kukufahamisha kwamba, kwa minajiri ya kuendeleza mahusiano yetu ya kikazi na wizara yako, kuanzia leo tumemteua mwandishi wetu mwadilifu Bw/Bi D.. M.. kuwa ndiye atakayekuwa na jukumu la kufuatilia kwa karibu shughuli za wizara yako kama sehemu ya dhima yetu ya kutoa habari kwa umma…”

Kwa upande wa vyanzo vya habari vya kati, mara nyingi mwandishi wa habari hahitaji kupewa kitambulisho. Jambo la muhimu ni kukuza mahusiano kwa misingi ya kusheshimiana, kukubaliana nia ya mawasiliano ambayo inahakikisha usiri kuhusu chanzo, na kukubaliana namna ambavyo habari uliyopewa bila serikali au vyama vya kitaaluma kujua itakavyoshughulikiwa.

  1. Vyanzo binafsi vya habari.Hivi ni vyanzo visivyojulikana au hata vya siri ambavyo waandishi wa habari wanavyo kati ya wasomi na watu wenye mamlaka makubwa. Wanapata vyanzo kama hivyo kwa njia ya kazi yao na maadili, wakiaminiwa na watu wenye habari isiyofahamika au iliyofichwa. Kamwe waandishi wa habari hawataji vyanzo vyao vya habari kwa mtu yeyote ikiwa ni pamoja na wakuu wao wa kazi; ni jambo lisilopingika kwamba mwandishi wa habari ndiye anayewajibika kwa habari anayopewa na vyanzo vyake.

Vyanzo vya habari vya kitaasisi + vyanzo vya habari vya kati + vyanzo binafsi vya habari = mtandao mzuri wa watoa habari.

  1. Vyanzo vya habari vya mara moja.Hivi ni vyanzo vya habari vya papo hapo, maelezo ya mashuhuda yanayotolewa au kuombwa kutokana na mazingira.Tahadhari ya kuchukua: bainisha chanzo; thibitisha makusudi yao; fikiria kwa kina kile wanachokisema; wafanye waeleze zaidi ya kile wanachotaka kukisema; linganisha kile walichokisema na vyanzo vingine vya kujitegemea. Ikiwa una mashaka, waombe wenzako maoni yao ya pamoja na ya kichambuzi endapo maelezo hayo yanapaswa kuchapishwa. Tilia mashaka vyanzo vya habari vinavyokupa kirahisi sana habari unayoitafuta.

KUWA GWIJI WA USAWAZISHO

Daima kuna haja ya usawazisho kati ya mwandishi wa habari na vyanzo vyake vya habari. Kunaupande“wenye kitu” – ule unaotoa habari, na upande “wenye uhitaji” – ule unaohitaji habari. Ni suala la ugavi na uhitaji… Kushughulikia usawazisho huu huhitaji stadi na ujuzi. Siku zote kuna shauku kwa upande wa chanzo cha habari kunufaika, ama binafsi au kitaaluma, kutokana na kutoa habari, kwa hiyo daima kuna hatari kwamba mwandishi wa habari anaweza kuchezewa akili. Mara nyingi kuna nafasi ndogo sana ya kuepuka hilo, lakini ipo. Ni suala la dhamiri. Usidanganyike. Usawazisho inabidi ufanyike.
Wakati mwingine “kujipendekeza” ni jambo zuri, na wakati mwingine si hivyo. Chanzo cha habari kinachobishana nawe ni bora kuliko msomaji aliyedanganywa.