MNAPOONGEA LUGHA MOJA, MNAWEZA KUBADILISHANA UJUZI.
LUGHA YA USANIFU
Habari (“paper”, “copy”): habari iliyoandikwa kwa ajili ya uchapishaji.
Mwegemeo wa habari: namna ambavyo mada inaanza kuandikwa.
“Lead”: sentensi ya kwanza au aya ya kwanza, inayolenga kumvutia msomaji.
“Body”: simulizi ya habari yenyewe, mpangilio wa kurasa za ndani, ukubwa wa vibambo.
Sentensi ya mwisho: hitimisho la habari, sentensi ya mwisho, aya ya mwisho.
LUGHA YA MTINDO WA UANDISHI
Maoni: habari fupi ambayo mwandishi anatoa maoni yake.
Habari fupi: habari fupi sana isiyo na kichwa cha habari.
“Bulletin”: maoni yasiyo na jina la mwandishi yanayoelezea msimamo wa gazeti.
Habari zinazogusa jamii: habari za matukio mbalimbali
“Column”: habari inayotoka baada ya muda maalum, iliyoandikwa kwa kwa namna ya uandishi wa mwandishi mwenyewe.
“Correspondence”: habari iliyoletwa na mwandishi maalum
“Wire story”: habari kutoka mashirika ya habari.
Udaku: habari fupi ya mambo ya kijamii.
Maoni ya Mhariri: maoni yaliyoandikwa na mkurugenzi au mhariri mkuu wa gazeti, mwandishi wa habari kutoka chumba cha habari au wakati mwingine mtu anayependa kuandikia magazeti.
Uchunguzi: ufichuzi, uchambuzi na uchanganuzi wa taarifa iliyopatikana kutoka vyanzo mbalimbali.
“Box”: aya fupi inayochomekwa kwenye maandishi kati ya mistari miwili ili kuvuta umakini wa msomaji.
Mahojiano: simulizi inayoelezea mahojiano, yaliyoandikwa kwa muundo wa maswali na majibu.
“Seasonal article”: habari ya mara kwa mara inayoongelea mada moja.
Wasifu wa marehemu: ripoti ya daktari ya uchunguzi wa kifo .
Ripoti: habari na ushuhuda wa kile kilichoonekana na kusikika huko mitaani .
Tangazo-habari (advertorial): tangazo linalotolewa kama habari.
Kigongo (scoop): habari ya kipekee ambayo ndiyo kwanza imetokea.
LUGHA YA UHARIRI
Kionjesho (kicker):mstari mfupi kwa kawaida juu ya kichwa cha habari unaoelezea habari kwa kifupi .
Vichwa vya Habari: vipengele vyote vinavyotengeneza kichwa cha habari .
Kichwa cha habari: maneno makuu ya habari .
Kichwa kidogo: usaidizi kwa kichwa cha habari.
Kibwagizo (inter): kichwa kidogo cha habari kinachowekwa ndani ya habari.
Jina la mwandishi: majina kamili ya mwandishi yanayowekwa juu au chini ya habari, kwa kirefu au kwa kifupi…
Maelezo ya picha: maneno yanayoelezea kielelezo.
Umiliki wa picha: jina la mpiga picha.
LUGHA YA UHAKIKI
Kosekano: neno moja au kadhaa yanayokosekana katika habari.
Neno lililokosewa: kosa la uandikaji sahihi wa neno.
Marudio: kosa la uandikaji linalosababisha neno, mstari, sentensi, nk kujirudia.
Kubadilisha maneno: kugeuza au kuchanganya herufi za neno.
Herufi: herufi ndogo inayotumika kuelezea ukubwa wa habari; idadi ya herufi kwenye habari ni idadi ya herufi ikiwa ni pamoja na nafasi za wazi.
LUGHA YA USANIFU
Safuwima kamili: habari inayoandikwa katika safuwima moja bila ya kukatwa na vichwa vidogo vya habari.
Kisanduku: maneno yanayozungukwa na kisanduku.
Kingo: mstari mnene au wa vitone unaotumika kutengeneza visanduku, au kutenganisha habari au maoni.
Kijachini: sehemu ya chini ya ukurasa.
Mlingoti: sehemu ya maoni ya mhariri.
Kichwa: sehemu ya juu ya ukurasa.
Kutoka: mwendelezo wa habari kutoka ukurasa wa mbele kwenda ukurasa wa ndani.
Kiwiliwili: sehemu ya kati ya ukurasa
LUGHA YA “DIRISHA”
Kihamasishi: maelezo kwenye ukurasa wa mbele kuhusu habari iliyoko ndani.
Bendera: sehemu ya juu ya ukurasa inayoonesha, kwenye ukurasa wa kwanza, jina la chapisho, na, kwenye kurasa za ndani, jina la sehemu, tarehe na ukurasa.
Habari Kuu: habari kuu kwenye ukurasa wa mbele ambayo inaendelea ndani.
Bango: kichwa ha habari kikubwa kabisa kinachotoka mwanzo hadi mwisho wa ukurasa.
Masikio: nafasi zilizo juu ya kila upande wa masthead.
Ufito wa chini: kichwa cha habari kikubwa sehemu ya chini ya ukurasa.
LUGHA YA UZALISHAJI
Kumaliza kazi: idhinisho la mwisho la kurasa kabla ya uchapaji
Kumalizia: usanifu wa mwisho wa ukurasa kabla ya “kumaliza kazi”.
Kipimo: ukadiriaji wa urefu wa habari.
Bamba: mwonekano kamili wa chapisho, unaoonesha habari na matangazo yalivyokaa kati ya ukurasa na ukurasa.
Mfano kamili: kurasa zote zilizoandaliwa.
L.S. (“Lala Salama”): ukurasa wa mwisho kuandaliwa wa gazeti.
Uthibitisho: mfano wa habari kamili iliyochapwa.
Karatasi: kipimo kikubwa zaidi kinachotumika kupima ukubwa wa habari; kina mistari 25 yenye herufi 60, pamoja na nafasi, yaani herufi 1500.
Nambari: nambari ya ukurasa.
Mfano: mfano wa ukurasa au gazeti zima.
Akiba: idadi ya habari zilizobaki bila kutumika.
Menyu: orodha ya habari zilizopendekezwa au kutunzwa au orodha ya kurasa zinazopaswa kukamilishwa.
Mpangilio: uwekaji wa vichwa vya habari, habari yenyewe, vielelezo na kingo za kurasa kama ilivyo kwenye mfano.
Muundo: mpangilio wa habari na picha kwenye ukurasa.
Umiliki: kisanduku chenye maelezo ya kisheria kuhusu umiliki na uongozi wa gazeti.
Habari motomoto: kurasa kwa ajili ya habari mpya kabisa.
Kurasa baridi: kurasa zinazoandaliwa mapema.
Yaliyomo: muhtasari wa maudhui ya gazeti.
LUGHA YA MAKATAZO
“Usiandike mkeka”: epuka kuandika habari kana kwamba unasuka mkeka…
“Usibwabwaje”: usitumie mistari 100 kuelezea kitu ambacho kingesemwa kwa mistari 10.
Usibuni mambo: kwa mwandishi wa habari kubuni habari ndiyo jambo la chini kabisa kulifanya.