Menu

05. Namna ya kuandika kwa usomaji wa kwenye skrini

Mwandishi wa habari anapoandika, ni kwa ajili ya kazi yake isomwe. Kama ilivyo kwa vyombo vya habari vya jadi (magazeti, redio na runinga), namna maudhui yanavyoandikwa lazima iwezeshe wasomaji kuyaelewa kirahisi kadri iwezekanavyo.

Kwenye skrini, msomaji lazima avutiwe kwa umakini.

Hii inaweza isieleweke lakini ni ukweli wa kisayansi: binadamu hawasomi magazeti kwa namna ile ile wanavyosoma maudhui ya kwenye skrini.

Wakati wa kusoma kwenye skrini, umakini hupungua sana, bila kuzingatia ukweli kwamba kuna mambo mengi sana yanayoweza kumsababisha kuondoa uwepo (hadharisho, arifu, jumbe, nk.). Moja ya madhumuni ya namna maudhui ya mtandaoni yanavyoandikwa ni kuvutia uwepo wa msomaji muda wote.

Kwa uhalisia, hii ina maana ya kutumia aya fupi, vichwa vya habari vingi vingi na uandishi rahisi. Kimwonekano, hii ni sawa na kupangilia vipande vidogo vidogo vya habari, kila kimoja kikiwa ni aya yenye wazo moja.

Maudhui ya midia-anuai (multimedia) hutoa vionjo mbalimbali kati ya maandishi

Kuvutia msomaji pia kunaweza kuwa kwa njia ya kutumia maudhui yasiyokuwa ya maandishi: picha, video, michoro, nk. Zana za uchapishaji mtandaoni zinazotumika na vyumba vya habari, mara nyingi huwezesha utumiaji wa michoro rahisi, na kufanya vipengele hivyo kujumuishwa katika habari. Hata hivyo, ni muhimu kuhakikisha kwamba unatumia tu maudhui ya midia-anuai ambayo una haki ya kuyasambaza.

Kiungo-wavuti (hyperlink), kipengele ambacho wasomaji wanakitarajia

Intaneti imejengwa kwa kutumia dhana ya viungo-wavuti. Kila unapotumia kivinjari cha intaneti, mara nyingi bila kutambua, unaperuzi kwa kubofya viungo hivi. Wasomaji wanatarajia kuona viungo hivi kwenye habari yako. 

Mtandaoni, pale jambo la ukweli linapotajwa, kiungo-wavuti cha habari inayohusiana na ukweli huo kinaongezwa. Pale waraka au video inapotajwa, kiungo-wavuti cha maudhui hayo kinaambatanishwa. Mbali na kuimarisha uaminifu unaohitajika kati ya msomaji na mwandishi wa habari anayenukuu vyanzo vyao, hiki pia ni kipengele muhimu cha Faniboresho ya Injini Tafuti (SEO), ambayo tutaiongelea katika sehemu ya 6.