Menu

08. Kuhakiki ukweli

Katika zama hizi za mitandao ya kijamii, habari za uongo na kupendelea kuamini mihemko, kuhakiki ukweli imekuwa mada muhimu kwenye vyumba vya habari.

Historia fupi ya kuhakiki ukweli

Kuhakiki ukweli ni utaratibu uliojitokeza Marekani katika miaka ya 1990 na mwanzoni ni utaratibu uliotumiwa zaidi na waandishi wa habari za uchunguzi. Baadae ulikua zaidi katika vyumba vya habari vya kidijitali kati ya mwaka 2000-2010 kupambana na habari za uongo zilizokuwa zimezagaa mtandaoni, kwenye mitanadoa ya kijamii na tovuti za nadharia ya njama, na hata wakati mwingien maneno yaliyosemwa na viongozi wa kisiasa.

Uingereza, karibu kila chumba cha habari kina waandishi wa habari waliobobea katika kuhakiki ukweli. Kwa kutumia zana za mtandaoni na mbinu madhubuti, wanafanya kila wawezalo kumaliza mijadala ambayo mara nyingi ni ya kitaalamu na migumu kuielezea. Timu zinzojulikana zaidi kwa kazi hii yawezekana ni Reality Check ya BBC na Full Fact, shirika linalojitegemea la Uingereza la kuhakiki ukweli. Pia kuna baadhi ya tovuti zinazojishughulisha tu na masuala ya dhana za njama, kama vile Snopes.

Kazi isiyo ya kisayansi sana ambayo kutoa jibu la “Sijui” ni jambo linalokubalika

Mbinu iayotumika katika kuhakiki ukweli inatumia utaratibu usio wa kisayansi sana unaotokana na mapokeo ya kiuandishi wa habari ya Uingereza, badala ya kufuata njia ya kisomi inayotumika katika tamaduni zingine, kama vile Ufaransa. Hakuna uoga, hakuna kuchukua misimamo ya kisiasa, hakuna tena kuwasilikiza wale wote wanaohusika katika jambo.

Kuanzia sasa na kuendelea, ukweli unatawala na ukweli ni jambo lililothibitishwa, hakika na linaloeleweka. Wahakiki wa ukweli wanategemea nyaraka tu (maandishi, vielelezo, picha, video, ripoti, nk.) kuthibitisha au kukanusha mambo yanayojadiliwa ndani ya kampuni. Ikiwa jambo haliwezi kupatiwa ufumbuzi, wanaendelea na uchunguzi wao hadi mwisho na kuwasilisha ugunduzi wao kwa umma, huku wakiwa tayari kukubali kwamba hawana majibu yote. 

Kuhakiki ukweli katika zama za habari za uongo

Ili kuweza kuhakiki ukweli, watu lazima waendelee kukubali kwamba wanawakilisha ukweli fulani. Katika zama hizi za kufuata mihemko ambayo imeshuhudia kuibuka kwa wimbi kubwa la dhana za njama, ni vigumu kwa wahakiki wa ukweli kufanya kazi yao kwa amani.

Katika miaka ya karibuni, kuhakiki ukweli ni jambo  ambalo limekuwa likikosolewa mara kwa mara. Zaidi ya hapo, ni jambo ambalo halikuwa na mchango sana katika kura ya maoni Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya (Brexit) au uchaguzi wa Donald Trump kama Rais wa Marekani, matukio mawili ambayo yaligubikwa sana na habari za uongo.