Menu

02. Kupangilia utafutaji wako wa habari

Ingawa mitandao ya kijamii ni vyanzo vizuri vya habari, injini tafuti, zikiongozwa na Google, nazo ni muhimu sana. Jambo moja ni hakika: haiwezekani kufuatilia kila kitu kinachochapishwa kila sekunde duniani kote. Ili kuepuka kuelemewa, lazima upangilie utafutaji wako wa habari.

Kutumia Google News na Google Alerts

Google News ndiyo sawa na meza ya kuuzia magazeti mtandaoni. Kuanza siku yako kwa kuperuzi Google News kamwe si wazo baya. Ni nzuri sana kwa kupata habari tofauti; hata hivyo, isisahaulike kwamba zana hii inaongozwa na “algorithm” na haijulikani vizuri ni namna gani “algorithm” hiyo inavyofanya kazi. Kukamilisha utafutaji huu wa habari tofauti, unaweza kutumia tovuti za kimaktaba kama vile CurationSoft. Tovuti hizi pia zinatoa habari tofauti lakini, wakati huu, zile zilizokusanywa kutoka mitandao ya kijamii.

Ikiwa maeneo yako ya kuandikia ni mahsusi, unapaswa kutengeneza Google Alerts. Weka neno msingi moja au zaidi na injini tafuti itakutumia barua pepe mara kwa mara ikiwa imeandaa tovuti zote mpya zenye maneno uliyoyaainisha. Hii ni njia nzuri ya kuhakikisha kwamba hupitwi na jambo la mada motomoto.

Kutengeneza orodha kadhaa kwenye Twitter na kuzipangilia kwa kutumia TweetDeck

Mitandao ya kijamii, hasa Twitter, ni vyanzo visivyokoma vya habari. Ikiwa unataka kudhibiti maudhui unayopata, ni muhimu kupangilia utafutaji wa habari tofauti kwa kutengeneza orodha za akaunti kuhusu mada zako (filamu, waigizaji, wanasiasa wa eneo fulani, wanasoka wa simu fulani, wabobezi katika nyanja fulani, nk.).

Ukishatengeneza orodha yako kwenye Twitter, kinachofatia ni kuziweka kwenye zana nyingine iliyotengenezwa an kampuni hiyo hiyo: TweetDeck. Faida kuu ya zana hii ni kwamba inakuwezesha kutazama mtiririko wa habari mbalimbali zinavyotokea (kulingana na wakati wa chapisho) kwenye skrini moja wakati huo huo. Ingawa hilo si zuri sana kwa matumizi ya simu-janja, zana hiyo inabaki kuwa muhimu ikitumika vizuri kwenye kompyuta.

Usisahau kuhusu majukwaa ya mtandaoni

Bila shaka, mitandao ya kijamii na injini tafuti, ambazo kwa sasa ni vinara katika ulimwengu wa habari, zina habari isiyoweza kuhesabika kwa kila sekunde. Hata hivyo, si mahali pekee unapoweza kupata ukitakacho. Kwa ujumla, majukwaa ya mijadala, ambayo yalikuwa maarufu sana katika siku za mwanzoni za intaneti, bado yanatumika.

Unataka kujua kile vijana wanachokiongelea? Tembelea jukwaa la tovuti ya UgandaNetworks. Je, unataka kupata uzi wa mjadala kuhusu mada fulani? Utapata kile unachokitafuta kwenye KenyaTalk. Katika miaka ya hivi karibuni, zana ya mijadala mtandaoni JamiiForums pia imekuwa na wafuasi wanaojadili mada kuhusu mambo yote. Kuna eneo kubwa sana la kushughulikia.