Menu

09. Kuripoti tukio mbashara

Kuna ufundi mahsusi wa kuripoti mtandaoni? Waandishi wa habari wa midia-anuai ni maripota kama wengine, lakini wanahitaji pia kuwa na hisia fulani za kwenda moja kwa moja na majadiliano, ambavyo ni vipengele muhimu kwa “kuripoti” tukio.

Kutumia picha mbashara

Intaneti ni chombo cha habari inayoendelea na kumbukumbu, inatoa uwezekano wa kuchapisha habari inayoweza kuwa na mwendelezo kadri muda unavyoenda. Kutoka “Tweet” ya kwanza yenye herufi 140 ikitangaza kuanza kwa maandamano hadi uchambuzi mrefu wa mafanikio (au kutofanikiwa kwake), intaneti inatumia miundo mbalimbali. Kutokana na unyumbufu na mwitikio wake wa haraka huifanya kuwa chombo sahihi kwa kuripoti matukio mbashara.

Kwa hiyo, ripota wa mtandaoni anaweza kufuatilia jambo kulingana na linavyotokea, bila ya kuwa na zana nyingine zaidi ya simu yake ya kiganjani. Kwa kutumia aina hii ya simu, unaweza kuchukua filamu ya kiongozi wa msururu, viongozi wa maandamano, kupiga picha zao, nk. Yote haya yanategemea wewe kuweza kutuma habari yako (maandishi na picha) na, kwa hiyo, ni muhimu kuwa na ufikio wa mtandao (simu) na kipimo-data (bandwidth) cha kutosha. Hii inahitaji kupiga video fupi fupi (zisizozidi dakika moja kwa urefu), au mfululizo wa picha ambazo ni rahisi kuzituma. Mara nyingi mitandao ya simu katika eneo la maandamano huzidiwa uwezo kwa sababu ya idadi kubwa ya mawasiliano yanayofanyika kwa wakati mmoja katika eneo dogo.

Mwisho, hakikisha hufanyi kosa la kizembe! Mapungufu makubwa ya kuripoti kwa aina hii ni kuharakisha kutuma kile unachoamini ndiyo habari kulingana na mtizamo wa haraka haraka au “kitu ulichokiona”. Kadri kunavyokuwa na utofauti mkubwa wa muda kutokea tukio hadi kuriripoti, ndivyo na uwezekano wa kufanya makosa unavyoongezeka.

Twitter Live

Kuripoti tukio mbashara kwa mfululizo wa jumbe zenye ukomo wa herufi 140 inahitaji uwezo mkubwa wa kufanya muhtasari na kipaji kisicho kifano kama msimulia hadithi.  Kazi hii inafanana na kuandika habari “Haraka” za mashirika ya habari: hakuna kurembaremba, hakuna kufuata vigezo vya uandishi na hakuna kucheza na maneno. Ni muhimu kusimama kwenye ukweli tu na si kingine isipokuwa ukweli, ukiheshimu mfumo uliozoeleka tangu zamani. Msemo ulioanzishwa na Pierre Lazareff (mmiliki mkubwa wa vyombo vya habari wa Kifaransa ambaye hakuwahi kuishi katika zama za intaneti) unaelekea kuwa sahihi kabisa kuhusu Twitter:

 “Sentensi ni nomino, kitenzi na sifa. Kwa kivumishi, nionye. Ukitumia tu kielezi, unafukuzwa kazi!” 

Ingawa Twitter inakuhamaisha utoe maoni yako, unapaswa kuchukua tahadhari kubwa kwa aina hii ya moja kwa moja ya kujieleza ambayo haijahaririwa. Hasa, epuka kutumia kejeli, ambayo inaweza kusababisha mtafaruku. Kejeli mara zote ni upanga wenye makali kuwili na tafsiri yake ni jambo tatanishi. Ikiwa imefichwa nyuma ya tungo yenye maana nzuri, mara nyingi kuna taswira tatanishi nyuma yake ambayo wasomaji wanasema wasiielewe au wakaitafsiri tofauti kabisa na namna ambavyo mwandishi alimaanisha.