Menu

24. Keeping an eye on upcoming developments

Intaneti inanbadilika kila wakati. Nani angedhani miaka 15 iliyopita kutakuwa na mitandao ya kijamii au majukwaa ya video mtandaoni? Kufanya kazi kwenye chombo cha habari ina maana pia kwenda sambamba na gunduzi mpya zinazoweza kubadilisha taaluma siku za mbeleni. Hii hapa ni mifano michache.

Utiririshaji, nyanja mpya kwa waandishi wa habari?

Twitch, jina hilo linakukumbusha chochote? Mtandao huu unawakutanisha mamilioni ya watazamaji kutoka kote duniani kila siku. Wanawafuatilia watu wenye shauku kama yao (kwa kawaida katika ulimwengu wa michezo ya video) kwenye video na mbashara kutoka eneo lao. Baadhi ya makampuni au makundi ya watiririshaji hata wametengeneza chaneli zenye vipindi maalum, kama vile tu vipindi vya runinga.

Maudhui ya mtandao huu yamebadilika katika miaka ya hivi karibuni kwa kuibuka kwa chaneli nyingi maalum kwa kuongea.  Chaneli moja maarufu ya habari inayojitegemea kwenye Twitch iliyo maalum kwa kujadili maoni ya kimaendeleo kuhusu masuala yanayomgusa kila mtu ni TYT.

Uhalisia Sibayana (VR), video za 360°

Ingawa video ndiyo njia inayoongoza mtandaoni, vumbuzi zinazotokea katika eneo hili daima ni jambo la kuliangalia kwa makini. Ukuaji wa video za simu za viganjani unaendelea, lakini vumbuzi kwa sehemu kubwa zinakuja kupitia teknolojia ya kisasa kabisa. Kuripoti kupitia 360° taratibu kunaanza kuzoeleka, hususan kutokana na kazi inayofanywa na Tool nchini Marekani.

Uhalisia Sibayana (Virtual Reality) bado haujaanza kutumika mtandaoni, lakini umeanza kwenye habari za runinga. Vifaa vinavyotumika kwa uandaaji wa uhalisia sibayana bado ni ghali sana, lakini vinaweza kuanza kupatikana kwa wingi katika miaka ijayo.

Akili bandia (AI)

Matumizi ya akili bandia tayari imeshakuwa maarufu katika vyumba vya habari vya Uingereza. Ilitumiwa, hususan, na BBC kwenye tovuti yao wakati wa uchaguzi mkuu wa hivi karibuni. Wataalamu wanakadiria kwamba siku si nyingi, maroboti sibayana yataweza kuandika asilimia 10 ya maudhui ambayo sasa huandikwa na binadamu. Hilo litawapa watu muda, wasemavyo wenyewe, wa kuandika habari ndefu na za uchunguzi. Itaendelea.