Menu

17. Kuandaa maudhui kwa ajili ya mitandao ya kijamii

Wakati meza za kuuzia magazeti ni sehemu za kupata magazeti, mitandao ya kijamii na sehemu za kupata maudhui ya mtandaoni yaliyoandaliwa na vyumba vya habari. Watumiaji wengi wa intaneti hawaendi tovuti za vyombo vya habari moja kwa moja. Kwa hiyo, ni muhimu kufahamu jinsi ya kuandaa maudhui kwa ajili ya jumuiya mbalimbali.

Kujua muda wa uchapishaji

Kuelewa vyema mitandao ya kijamii ina maana kuelewa ni wakati gani mzuri zaidi wa kuchapisha maudhui. Kwa ujumla, inaweza kuzingatiwa kwamba wakati wa saa za kazi, hadhira inakuwa ndogo. Ni wakati wa chakula cha mchana na alasiri ndipo watu wengi huingia mtandaoni. Hizi hapa ni baadhi ya data za kina:

Kwenye Facebook, inashauriwa kuchapisha maudhui yako yapata saa 3:00 asubuhi au wakati wa chakula cha mchana, kati ya saa 7:00 na saa 9:00. Kwenye mtandao huu, kwa ujumla utakuwa na mafanikio zaidi siku za mwisho wa wiki.

Kwenye Twitter, wakati wa chakula cha mchana, hasa Jumatano, ndiyo muda ambao watu wengi huingia mtandaoni. Unaweza pua kuchapisha maudhui mara kadhaa wakati wa mchana.

Kwenye Instagram, juhudi zielekezwe asubuhi, kati ya saa 2:00 na saa 3:00, na mwisho wa siku, wakati watu wote wanaporudi nyumbani baada ya kazi. Kwa vile mtandao huu wa kijamii unatumia zaidi picha, daima ni bora zaidi kuchapisha video kuliko picha kwa matumaini ya kuwafikia watu wengi zaidi.

Utangulizi kwa dhana ya uhusishaji

Kwa ujumla, mitandao ya kijamii ni mahali pa kuhusiana na jumuiya yako. Ikiwa unataka kukuza hadhira yako, inabidi utengeneze kiungo, changamoto, kuuliza maswali, kupendekeza tafiti, kujibu maswali, nk. katika vyumba vya habari vya vikubwa, kazi hii ya uongozi kwa kawaida wamepewa mameneja jumuiya, ambayo ni nafasi mpya inayolenga kukuza mahusiano na hadhira.

Nafasi hii inakuwa muhimu zaidi kwa vile mitandao ya kijamii, ikiongozwa na Facebook, mara nyingi hufanya kwa kutumia “algorithm” zinazoonesha zaidi maudhui yaliyoandikwa vizuri sana yenye picha au kielelezo. Ikiwa maudhui yako yaliyochapishwa yatavutia wengi, yatapendwa, na kutolewa maoni na kushirikishwa, utakuwa na uwezekano mkubwa wa kuoneshwa zaidi katika mtandao huo. Kukuza uhusishaji wa hadhira ina maana kufanikiwa kuongeza mwingiliano kati ya maudhui yako yaliyochapishwa na jumuiya yako.

Kutambua jinsi maudhui yanavyotumika

Ili kufanikiwa kwenye mitandao ya kijamii, bila shaka ni muhimu kujua muda wa kuchapisha maudhui yako mtandaoni, lakini kuelewa mazoea ya namna gani yanatumiwa ni muhimu.

Hebu tuchukue mfano wa mafanikio ya chombo cha habari kiitwacho Brut. Watengenezaji wa shirika hili mwanzoni walivutiwa na namna video zilivyokuwa zikiangaliwa mtandaoni. Walibaini kwamba video nyingi zilizoangaliwa zilikuwa fupi na mara nyingi zisizo na sauti. Kutokana na uchambuzi huu walitengeneza muundo wa kuweka maandishi moja kwa moja kwenye video na maelezo mafupi. Muundo huu sasa unatumika karibia katika kila chumba cha habari.