Menu

21. Kufanya habari kuwa burudani

Kujifunza huku ukiburudika? Kwa nini isiwe hivyo. Kwa miaka kumi iliyopita au zaidi kidogo, michezo na ucheshi vimeingizwa kwenye maudhui muhimu ya uandishi wa habari kuwawezesha wasomaji kuelewa vizuri zaidi vipengele vya habari.

Tangu chemsha bongo hadi mchezo mgumu: kuburudika huku ukijifunza

Huhitaji mchezo wa video ulio mzuri ili kuburudika. Pengine umeshakutana na chemsha bongo ya habari iliyowekwa kwenye tovuti ya chombo kikubwa cha habari cha mtandaoni. Hapo ndipo kuifanya habari kuwa burudani huanzia. Aina za michezo ziko nyingi na zinaweza kuchukua siku chache hadi miezi kadhaa kuitengeneza.

Katika muundo wake mgumu kabisa, ufanyaji habari kuwa burudani huchukua muundo wa “mchezo mgumu” au “mchezo wa habari” Hiyo ya mwisho ipo kati ya uandishi wa habari na michezo ya video. Kwa ujumla mtu humchezesha mhusika mwenye shani fulani itakayodumu kwa muda mrefu. Juhudi inawekwa katika michoro na usanifu wa mchezo huo.

Mifano michache mizuri

  • Activate: fanya kampeni ya suala la chaguo lako, kuza mtandao wa marafiki kuwa wimbi la kitaifa, husisha jumuiya na viongozi wako mahalia ili kukuza uelewa na kuunga mkono harakati zako..
  • The Political Machine 2020: ongoza kampeni ya kumchagua Rais wa Marekani.
  • Branches of Power: Chagua viongozi kwa kila mhimili wa serikali, andaa ajenga ya urais, peleka miswada na pitisha sheria Bungeni, sikiliza kesi za sheria zilizotungwa bungeni.