Menu

13. Uoneshaji wa data

Baada ya kuibuka uandishi wa habari kwa kutumia data, fani nyingine nayo imekuja kumea kabisa katika nyanja ya habari: uoneshaji wa data. Au jinsi ya kuonesha data ngumu na ya kiufundi kwa namna ambayo inaweza kueleweka mara moja tu.

Kupangilia data na kuitofautisha kwa rangi

Kuamua ni data ipi unataka kuionesha ni jambo moja, kubaini namna sahihi ya kuionesha data hiyo ni jambo lingine. Katika eneo hili, hakuna jibu la moja kwa moja na kama ukibahatika kufanya kazi na msanifu daima unaweza kupata fumbuzi za papo hapo za namna ya uoneshaji wa data yako.

Baada ya kusema hivyo, vyumba vya habari si wakati wote zina fedha za kutosha kuajiri wataalamu wa namna ya uoneshaji wa data na utahitajika kujua kanuni chache za msingi kuhakikisha kwamba huwapotoshi wasomaji wako.

Chagua uoneshaji  wako wa data kwa umakini

Hebu tujadili muundo kabla ya yote. Ugawaji, mabadiliko kulingana na muda na matokeo ya kura hayaoneshwi kwa namna moja. Njia rahisi zaidi ya kubaini jinsi ya kuonesha data ulizonazo ni kutumia zana hii iliyotengenezwa na gazeti la Financial Times.

Hakuna sheria zisizopindika inapokuja kwenye suala la rangi utakazotumia katika uoneshaji wako wa data, lakini hekima kidogo tu huwa haina madhara. Hebu tutumie mfano wa matokeo ya uchaguzi. Kama unaonesha data ya urari wa kisiasa bungeni, mara nyingi ni wazo zuri kuonesha wanasiasa wa mrengo wa kushoto kwa rangi ya pinki au nyekundu, wanasiasa wa mrengo wa kulia kwa rangi ya bluu na wanamazingira kwa rangi ya kijani. Jaribu kuchanganya rangi hizi na utaona kwamba uoneshaji wako wa data hautaeleweka.

Zana chache ambazo ni rahisi kutumia

Kuna zana kadhaa za bure mtandaoni ambazo unaweza kuzitumia kujaribisha uoneshaji rahisi wa data. Datawrapper, zana iliyopangiliwa vizuri na rahisi kutumia, inatumika katika vyumba vya habari vingi kwa ajili ya uoneshaji wa data ya ukosefu wa ajira na mchanganuo wa bajeti ya kila mwaka.

Infogram ni ngumu zaidi kuitumia, lakini itakuwezesha kufanya zaidi ya uoneshaji rahisi wa data. Utakuwa na uwezo wa kutengeneza maudhui yenye maandishi, video, nk.