Menu

07. Kutumia rasilimali za picha na kusimamia hakimiliki ya picha

Baada ya maandishi, uandaaji na matumizi ya picha ndiyo mbinu iliyozoeleka zaidi katika kuipa habari vielelezo. Kuna rasilimali nyingi zinazopatikana mtandaoni. Baadhi ya hizo zinatumiwa huria; hata hivyo haina maana ni za bure.

Kushirikishana picha kwenye majukwaa ya kushirikishana

Kuna idadi kubwa ya majukwaa ya kushirikishana picha, huku yanayojulikana zaidi yakiwa: FlickR, Photobucket, Fotolia, nk. Baadhi yanaruhusu kuchapisha picha bila malipo, wakati mengine yanatoza gharama. Kwa vile kazi yetu, kwa sehemu fulani, inategemea kuuza habari, ni busara na jambo jema kuheshimu kanuni zote zote za kisheria zinazohusika na uuzaji wa picha.

Hakika, usishawishike kuiba picha kutoka kwa mmiliki wake halali, ambaye hatimaye atakugundua na na kwa haki kudai malipo yake! Ikitokea kwamba huna fedha, kuna idadi kubwa ya picha zenye ubora wa hali ya juu ambazo hazina hakimiliki na zinaweza kuchapishwa bure. Ndivyo ilivyo pia kwa picha na video zinazopatikana kwenye mitandao ya kijamii. Mara nyingi ni jambo jema kuwasiliana na mwenye nazo kumwomba idhini ya kuzitumia.

Creative Commons

Chukua Flickr kama mfano, moja ya majukwaa yanayopokea maudhui yake kutoka kwa watumiaji wa intaneti, wanaoamua kupakia maudhui yao chini ya leseni ya Creative Commons. Kuna aina sita tofauti za leseni hii, kuanzia kutumia bila malipo ambayo haina gharama yoyote, ilimradi kwamba mwenye picha anatajwa, hadi matumizi yaliyozuiwa ambayo kuna gharama inatozwa, kulingana na masharti fulani na kutoruhusu kufanya marekebisho yoyote kwenye picha.

Mbali na mfumo huu, sheria ya hakimiliki inatumika katika sehemu mbalimbali za dunia, ambayo inahusisha kupata idhini ya kuchapisha picha kutoka kwa mwenye picha, kwa malipo na chini ya masharti yaliyoelezwa bayana kuhusu muda na eneo.

Hebu turudi katika Creative Commons. Kwenye Flickr, unapofanya utafutaji, utaona neno linatokea juu kushoto ya skrini yako linalosema “Any licence”, ikiwa na maana una leseni?. Bofya hapo na chagua “Commercial use allowed” kuhakikisha kwamba unaona tu zile picha ambazo unaweza kuzitumia bila kutaja hakimiliki. Ukitaka kuwa na uwezo wa kuifanyia marekebisho picha, chagua “Commercial use & mods allowed”.

Kuhariri picha

Baada ya kuhakikisha kwamba picha iliyochaguliwa inaweza kufanyiwa marekebisho, kuna programu mbalimbali za kuhariri zilizopo kufanya picha iendane na muundo wa chapisho lako. Ama kompyuta yako tayari inaweza kuwa na programu stahiki, au unaweza kuchagua programu ya bure GIMP au huduma ya mtandaoni iitwayo Pixlr.

GIMP kwa hakika ndiyo yenye uwezo mkubwa zaidi kati ya programu hizi. Hasa, inakuwezesha kubadili ukubwa wa picha yako, ili kuepuka kuweka data kubwa kwenye maudhui, ambayo itachelewesha muda wa upakiaji wa ukurasa. Kadri picha inavyokuwa na data kubwa zaidi, ndivyo itakavyotumia muda mwingi zaidi kupakia.

Huu ndiyo utaratibu wa kufuata kwenye GIMP, baada ya picha kupakiwa kwenye programu:

Kwenye tabo ya “Image” nenda kwenye “Scale Image”.

Ukubwa wa picha unaoneshwa kwa kutumia vigezo viwili, “Upana” na “Urefu”. Unapobadilisha kigeo kimoja, kingine kinabadilika kiotomati, kulingana na uwiano halisi wa picha.

Ukishaamua ukubwa wa kutumia, bofya “Scale” kuona matokeo, kisha hifadhi picha yako kwa kwenda kwenye tabo ya “File”.

Tafadhali zingatia kwamba ukubwa wa skrini ya kwaida ni pixel 320 kwa simu ya kiganjani, pixel 1024 kwa kompyuta mpakato na pixel 1440 kwa skrini ya Kompyuta kubwa ya mezani. Mtandaoni, ukubwa mzuri ni kati ya pixel 600 na 800.