Menu

01. mpangaji wa siku moja wa

Waandishi wa habari wana ugonjwa wa shauku: nini kipya duniani? Wana uhitaji mkubwa sana wa kupata “habari” ambazo huwapa watu. Wanahitaji kujua kinachoendelea katika mazingira yao ili waweze kuwapasha habari watu wengine. Hata hivyo, kazi yao kama wasema ukweli huwalazimu kutenganisha habari za kweli na zile za uongo ili kuhakikisha kwamba wanasambaza taarifa za kweli. Hufanya hivyo kwa kutunza orodha ya “habari” za kweli au zilizothibitishwa katika shajara.

SHAJARA ILIYOPANGILIWA VIZURI = GAZETI LENYE UBORA

Ubora wa maudhui ya gazeti unawiana na yale yaliyomo kwenye shajara. Shajara madhubuti imegawanywa katika sehemu tatu:

 Ratiba ya habari za hivi punde: orodha ya matukio ya kila siku ya yaliyotengazwa siku hiyo na vyanzo vinavyofahamika. Humwezesha mwandishi wa habari kujiandaa jinsi atakavyoshughulikia mambo yanayotokea kila siku. Kwa mfano: “Naandaa habari ya safu moja na nusu kesho kuandika kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu itakayotolewa mchana huu”.

Ratiba ya habari tarajiwa: nini kinahitaji kufanyika ili kushughulikia habari zijazo katika kipindi cha muda mfupi, wastani na mrefu. Huwezesha habari zijazo kuandikwa kabla.

Kwa mfano: Nahitaji kuandaa vikao kadhaa ili kutathmini hali ya kijamii kuelekea maadhimisho ya ghasia za mwaka jana.

Ratiba ya habari teule: mada binafsi zilizoongezwa thamani zaidi. Hilo humwezesha mwandishi wa habari kujumuisha mada zinazolenga kuunga mkono au kupinga habari zinazoibukia au tarajiwa katika programu zao.

Kwa mfano: “habari hii inahuzunisha, nakwenda kumhoji yule muuza duka mdogo na anayejitegemea kwenye kona ambaye mara zote yeye huwa mcheshi…”.

Wakati mkifanya kazi kama timu, shajara ya pamoja ni bora kuliko shajara binafsi.

MADIRISHA MATANO YA KUFUNGUA KILA SIKU

Jambo la kwanza ambalo mtafiti wa “habari” lazima alifanye kila siku ni kufungua madirisha ambayo yanayoangazia maeneo ya habari.

Kuna madirisha matano ya asili: redio, runinga, intaneti , magazeti  na  baa au mgahawa mahalia.

Naelewa mambo yanayotokea kila siku kwa kusikiliza redio, kutazama runinga, kuperuzi mtandao, kusoma habari mpya na kusikiliza kile watu wakisemacho katika baa, mgahawa au duka mahalia. Hivyo naamka mapema.

Nidhamu hii ya kila siku huwawezesha waandishi wa habari:

  • Kuboresha shajara zao kwa kujumuisha michango kutoa vyombo vingine vya habari kwenye mipango yao.
  • Kutathmini kazi yao binafsi kwa kuilinganisha na ile ya wenzao. Kujenga hali ya kujikosoa ambayo huwakinga wasiingie katika mtego wa kuridhika.

KUANDIKA VIDOKEZO = ONGEZEKO LA THAMANI

Jambo la pili ambalo waandishi wanaotaka kuboresha utendaji wao wa kiweledi lazima walifanye kila siku ni  kuhifadhi michango kutoka vyombo vingine vya habari. Kulinganisha kazi yangu na ile inayozalishwa na wengine huboresha ufahamu wangu wa mada ninazoziandika ndani ya wigo wa wajibu wangu. Kuandika vidokezo bora huzalisha habari bora.

Unachohitaji ni mkasi tu ili kukata na kuhifadhi dondoo kutoka magazeti ya kila siku, ambazo, zikikusanywa na kuhifadhiwa kwa mfuatano wa matukio au kulingana na maudhui, huunda maktaba binafsi kwa mwandishi wa habari anayetafuta kuwa na uandishi bora zaidi.

MTEGO WA KUEPUKA

Shajara haipaswi kamwe kuchukuliwa kama injili. Kamwe haijumuishi uhalisia wote. Kwa hiyo waandishi wa habari  wanaweza kuingia kirahisi kwenye mitego ikiwa wataruhusu kanuni za kuandaa shajara zitolewe kwao na wataalamu wa mawasiliano.

SWALI LA KUJIULIZA

Baada ya kutafakari namna mbalimbali ambazo naweza kuifanya shajara yangu kunipa vichwa vya habari, najiuliza swali moja la mwisho: ni nini zaidi nachoweza kufanya au ni nini naweza kufanya vizuri zaidi ili kufanya maudhui ya gazeti langu yaelimishe zaidi kuliko maudhui ya wengine?