Ramani za “choropleth”
Bila shaka hii ndiyo aina ya ramani inayotumika mara nyingi katika magazeti, pengine kwa sababu ndiyo rahisi zaidi kutengeneza. Ramani za “choropleth” zinakuwezesha kupaka rangi kwenye ramani ya maeneo mbalimbali ya utawala kulingana na kipande husika cha data.
Kwa mfano, ukitaka kutengeneza uoneshaji wa data ya idadi ya Watanzania kulingana na wilaya, wilaya zenye watu wengi zaidi zitakuwa na rangi iliyokolezwa na zenye watu wachache zitakuwa na rangi iliyopauka.
Ramani za “heat”
Safari hii, hutatengeneza kipimo cha rangi kulingana na kipande cha data. Jambo muhimu hapa ni kuonesha, ndani ya hifadhi-data, anwani, maeneo au anwani za kijiografia jambo lilipotokea. Na ni mjumuiko wa pointi hizo ambao utatengeneza umbo kwenye ramani.
Mfano mmoja ni kazi inayofanyika Scotland kubaini maeneo ya hatari kwa waendesha baiskaeli mijini. Kila pointi inawakilisha mahali ambapo ajali ilitokea. Kwenye ramani, mjumuiko wa pointi unaonesha mahali pa hatari kwa waendesha baiskeli.
Ramani za “anamorphic”
Kulingana na ufundi, ramani za “anamorphic” ndiyo ngumu zaidi kutengeneza. Kuhusiana na data, zinafanya kazi sawa sawa na ramani za “choropleth”: kipande cha data kinahusishwa na eneo la kijiografia. Tofauti ni kwamba badala ya kuweka rangi tofauti eneo la kiutawala linalohusika, programu ya kompyuta inaifanyia mabadiliko kiasi. Tukirudi kwenye mfano wa awali wa idadi ya watu wa Tanzania, ramani ya “anamorphic” inaonesha maeneo muhimu zaidi ya idadi ya watu katika nchi ukiiangalia tu.