Menu

11. Kutengeneza simulizi

Snapchat, Instagram na hata TikTok ndiyo hasa ulimwengu wa simulizi, zile video fupi zisizodumu muda mrefu. Zikiwa maarufu sana kwa watumiaji vijana, simulizi hizi zinaonesha njia mpya ya kuelezea jambo ambayo ina mwitikio na inaendana na matukio yanayotokea sasa.

kuna tofauti gani kati ya video zilizozoeleka na simulizi?

Simulizi ni picha au video fupi unayoiweka kwenye akaunti yako ya Snapchat, Instagram au Facebook na kwamba rafiki/wafuasi wanaweza kuitazama kwa saa 24. Baada ya hapo, inatoweka. Maudhui hayo hayadhamiriwi kubakia mtandaoni na kwa hiyo hilo halihitaji kufanya uwekezaji unaotakiwa katika kupiga video na kuzihariri kitaalamu.

Kimsingi, kutengeneza simulizi ina maana kwamba hilo litaendana na habari kwa sababu itapotea kesho yake tu. Kwa hiyo ni zana ya mwitikio mkubwa ambapo vipengele vya kimuktadha mara nyingi vinaweza kuongezwa, ambavyo vinaweza kuunganishwa na vipengele vingine mtandaoni.

Kuifikia hadhira yako moja kwa moja na kwa lugha isiyopinda-pinda

Mitandao ya kijamii ambayo inajumuisha kipengele hiki cha simulizi ni maarufu hasa kwa vijana. Mitandao hii ina kanuni na utamaduni wake. Kwenye mitandao hii ni lazima kutengeneza jumuiya, kuhusiana na wafuasi wako na kujibu maswali yao. Kwa hiyo maudhui yanayotengenezwa yanaakisi ukaribu huu na hadhira yako. Usisite kuipa hadhira yako changamoto na kuomba mwitikio wao (kama vile kupitia maoni, kwa mfano).