Uhakikisho wa picha kwa kutumia Google Image
Google inakuwezesha kufanya utafutaji wa maandishi, lakini si utafutaji wa maandishi tu. Kwa kutumia zana ya Google Image, unaweza pia kutafuta iwapo picha uliyonayo imeshatokea kwenye intaneti. Hii inaweza kuwa ya manufaa katika mazingira ambayo chanzo kinasema, kwa mfano, kwamba picha hii ni ya hivi karibuni.
Kufanya uhakikisho huo, nenda kwenye tovuti ya Google Image. Chukua picha kutoka kwenye kompyuta yako na iweke kwenye upau wa utafutaji. Baada ya hapo Google itakuonesha kurasa zote zenye picha hiyo. Kwa njia hiyo utaweza kuangalia tarehe ya uchapishaji wa habari zenye picha hiyo.
Ikiwa Google haiwezi kutoa jibu sahihi, hilo huelekea kuonesha kwamba hakika picha hiyo ni ya karibuni. Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia kwamba zana hii inakuhakikishia tu kwamba picha hiyo haijawahi kuchapishwa mtandaoni. Ikiwa bado una mashaka, yumkini unaweza kuendelea na uchunguzi wako kwa kutumia mbinu zilizozoeleka zaidi.
Data za EXIF na IPTC za picha
Mafaili ya picha, kama aina nyingi za mafaili, wakati mwingine hujumuisha data zilizofichika: hizi zinaitwa metadata. Data hizi kwa kawaida ni za kiufundi: modeli ya kamera iliyotumika, kasi ya kupiga picha ya kifaa, nk. Baada ya kusema hivyo, unaweza kupata data za manufaa sana kwa kubaini chanzo cha picha.
Data za EXIF au IPTC wakati mwingine zina taarifa kama vile jina la mpiga picha na muda na tarehe picha ilipopigwa. Ukiwa na bahati kidogo, unaweza hata ukapata anwani ya kijiografia ilipopigwa picha au aina ya ukerebishaji uliofanywa kwenye picha halisi. Hivi vyote ni vipengele vya ziada vinavyokuwezesha kuhakikisha ukweli wa kile unachokiona.
Kila aina ya programu ya kutengeneza picha ina namna tofauti ya kupata metadata ya picha. Utafutaji kwenye intaneti kwa kiasi kikubwa hukuwezesha kupata ufumbuzi wa unachokitafuta. Ukitumia Photoshop, bonyeza Ctrl+Alt+Shift+J (au Cmd+Alt+Shift+J kwenye Mac) na metadata itatokea.
Kutambua video ambayo imeshasambazwa huko nyuma
Kuchunguza video ni ngumu kidogo. Hata hivyo, kuna zana zinazoweza kukusaidia. Shirika la Amnesty International limetengeneza zana ya kukusaidia kubaini iwapo video ya YouTube imeshasambazwa kwenye mtandao au la.
InVid ni nzuri na ya kiufundi zaidi, ambayo kimsingi imelenga kuwasaidia waandishi wa habari wanaotaka kuhakikisha picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii. Mahsusi, inawezesha utafutaji wa kuhakikisha ikiwa video iliyowekwa Twitter, Facebook, YouTube, Instagram, Vimeo, Dailymotion, LiveLeak na Dropbox ilishasambazwa mtandaoni kabla.