Menu

16. Kuandaa muundo wa kipindi kirefu na ingiliani

Kuanzia makala za mtandaoni hadi habari ndefu, intaneti imejaa miundo bunifu ya uandishi wa habari. Ingawa mara nyingi zinasifiwa na wachambuzi na wasomaji, hata hivyo ni kazi kubwa sana kuziandaa na hata kuzifanya zizalishe faida.

Suala dogo la msamiati

Kama jina lake linavyodokeza, makala ya mtandaoni ni makala ingiliani kwa ajili ya kuangaliwa kwenye intaneti. Ikiwa maarufu sana mwanzoni mwa miaka ya 2010, lengo ni kumshirikisha kwa kina msomaji katika mazingira yanayoelezewa na makala ya mtandaoni. mfano mmoja wa iliyofanikiwa zaidi pengine ni  Fort McMoney ya David Dufresne.

Habari ndefu ni makala ya muundo wa kuburudisha inayopendelewa sana na vyombo vya habari vikuu pale vinapotaka kuipa habari kipaumbele. Habari ndefu zinatumia muundo uliozoeleka sana, lakini kwa kawaida huboreshwa kwa picha, vikaragushi kwenye ramani, video zilizowekwa kwenye habari, nk. kazi inayofanywa na Longreads kwa miaka kadhaa sasa ni mfano mzuri wa muundo wa habari ndefu.

Kufanya kazi kama timu

Ni waandishi wa habari wachache wenye uwezo wa kuandaa peke yao makala ndefu na ingiliani. Matoleo haya ya mtandaoni kwa ujumla huhitaji ujuzi wa ziada mbali na ule wa mwandishi wa habari. Zinahitaji msanidi programu kusanidi habari hiyo kwenye ukurasa wa tovuti, msanifu michoro kuweka urembo, na wakati mwingine mtayarishaji video na wakati mwingine mtunzi.

Kwa ufupi, kuandaa makala ndefu na ingiliani mara nyingi ni fursa kwa mwandishi wa habari kujifunza stadi nyingine. Unapoanza mradi wa aina hii, inashauriwa kuwa na wasaidizi madhubuti na, hasa, usitegemee kumaliza haraka sana.

Uchumi mbaya kiasi

Tatizo ni kwamba vyombo vya habari kwa ujumla havina uwezo wa kutenga rasilimali za kutosha kwa miradi ya aina hii kwa kipindi cha muda mrefu. Licha ya jitihada nyingi, ni miradi ingiliani michache ndiyo imeweza kuvutia hadhira au kufanya kufanya mradi wao utoe faida.