Menu

03. Ni nini mada?

Redio haiwezi kusema yote, habari zinamipaka kulingana na muda uliopo, inabidi kwa hiyo kuchagua. Suala la mada inatupeleka kwenye suala inayousiana na ripoti. Mwandishi wa habari anaweza kugusia mada mbali mbali. Kila mada ianweza kutangazwa, kuangazwa kwa mujibu wa masuala mbali mbali.

Mada, changuo la kiuwandishi wa habari.
Kila siku, vyombo vya habari vinagusia mada muhimu. Kila chombo cha habari kinaweza kugusia mada ile ile kwa mitazamo tofauti. Inategemea mada iliyochaguliwa na inavyochambuliwa. Kama mada ni nzuri, ripoti itakuwa ya kuvutia.

Mada: Jibu juu mambo yanayosumbua kazi ya uwandishi wa habari.

Ni muhimu kutoa taarifa zote kwenye karatasi ya dakika moja. Mwandishi wa habari wa redio analishugulikia hilo na kuweka kila kitu mezani. Chaguo la mada nzuri inasaidie ripoti inayobidi kurushwa. Hakuna kinachowakataza kugusia jambo yenye mada mbili tofauti: Kutoa mada kwenye habari za jioni na pili habari ya kesho yake asubui.

Wakati gani kutambua mada ?

Wakati wa kuchagua mada ya jambo au taarifa yeyote, ni wakati wa mkutano wa mhariri, waandishi wa habari na habari zitakazo rushwa: Jinsi gani tutagusia kila mada, ni kipi ambacho kinawavutia wasikilizaji kwenye mada hii, ni nani ambao ni wazungumzaji wazuri kwenye mahojiano? Kuweza kujibu mawali haya ni wakati wa mkutano wa asubui na timu nzima.

Mifano ya mada

Tuchukue mfano wa habari: moto unatokea kwenye mtaa moja jijini unapoishi, nyumba na maduka yanawaka moto. Hapa baadhi ya mifano ya mada zinazoweza kugusia kwa mijibu wa habari iliyopo.

  • Mada ya kwanza: Kumtuma ripota kwenye eneo la tukio ambaye tutazungumza naye kwa njia ya simu akifafafanua tukio ilivyo. Ufanyaji Kazi: Taarifa kamili kwa njia ya simu.
  • Mada ya pili: Kutoa ripoti juu ya hali ya vifaa vilivyoteketea na wanadamu: watu wangapi waliofariki, waliojeruhiwa, jinsi gani huduma ya kuwakomboa inaratibiwa, mitaa mingapi, nyumba zimehathirika, n.k. Ufanyaji Kazi: mahojiano mafupi na kiongozi wowote.
  • Mada ya tatu: Elezea kile kilichotokea. Wakati gani na wapi moto umeanza? Kwa sababu gani? Je, ni moto uliokusudia au ni ajali. Ufanyaji Kazi: Habari fupi studio.

Tunaweza kuchagua kati ya mada mbali mbali. Tunaweza mada nyingi kwa ajili ya kubadilisha ripoti kutoka chombo kimoja cha habari hadi chombo kingine. Kama tukio ni muhimu sana, tunaweza kuipa mada nyingi ndani ya habari moja na kuitengenezea jalada.

Kanuni inatumika kwa kila tukio, siasa, utamaduni, uchumi, michezo (habari ya kusomwa kabla ya mechi, taarifa ya kabla ya mechi, taarifa ya baada ya mechi, mahojiano na wachezaji, kocha na karatasi ya mahojiano…)

Vile vile kwa ajili ya kesi fulani: Karatasi ya kumbukumbu ya matukio mbali mbali ya kesi, kumtambulisha mtuhumiwa, karatasi inayofupisha kesi, taarifa kamili na mawakili wa pande zote mbili.